Loading...

NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA

Loading...
NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA
link : NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA

soma pia


NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA

Mkazi wa kata ya Kakonyo, Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Bwana Faraja Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii jinsi alivyopigwa na kuumizwa na wafugaji wa nchini Uganda kwa kosa la kukamata mifugo ya waganda iliyokula mazao ya wananchi wa Tanzania katika kijiji hicho mwaka 2016 (Picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi).

Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Nape Nnauye ameishauli Serikali kuboresha mipaka ya nchi kwa wakati ili kuondokana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara kufuatia uvamizi wa wahamiaji kutoka nchi jirani.

Ameyasema hayo katika ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembea mipaka kati ya Tanzania na Uganda Wilaya ya Missenyi upande wa Tanzania Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Isingiro upande wa Uganda.

Nape amesema suala la kulinda mipaka ni muhimu hivyo ni vyema serikali kupitia Wizara ya Ardhi ikatenga fedha za kutengeneza barabara zilizoko mipakani ili kurahisisha ulinzi na usalama wa mipaka yetu na kuwezesha wakazi wa nchi hizi mbili kutambua mipaka ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua mpaka wa Tanzania na Uganda katika eneo la mto kagera.

“Tumebaini kuwa kuingia kwa wananchi wa Uganda hasa kuleta mifugo yao katika lanchi ya Missenyi kunachangiwa na kutokuwepo njia maalumu na alama maalumu zinazotenganisha kati ya nchi na nchi hivyo watu wanaingia kupitia katika vichochoro visivyo rasmi na kuhatarisha amani kwa wakazi wa mipakani alisema Nnauye”

Kamati hiyo pia ilifanikiwa kufika katika vijiji vya Rwengiri, Bwenkoma na Bubale vilivyopo kata ya Kakunyu na kubaini kuwa baadhi ya alama zilizowekwa mpakani zimepotea hivyo wafugaji kutoka maeneo mbalimbali wanaendelea na shughuli za ufugaji bila kujali sheria.

Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa ikikagua mipaka na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kama barabara itatengenezwa katika mipaka yote ya Missenyi kazi ya kuwabaini waarifu itakuwa rahisi.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Dkt. James Mtamakaya akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii mipaka iliyopo kati ya Tanzania na Uganda.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa mpaka sasa Wizara imepokea shilingi bilioni 4 za kuimarisha mipaka ambapo fedha zitakazotumika kuimarisha mpaka wa Tanzania na Uganda ni shilingi Bilioni 1.9 na shilingi Bilioni 2.1 kwa mpaka wa Tanzania na Kenya.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Hivyo makala NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA

yaani makala yote NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/nape-aishauri-serikali-kuimarisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA YA NCHI HARAKA"

Post a Comment

Loading...