Loading...

NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake

Loading...
NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake
link : NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake

soma pia


NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake

Na Grace Michael, Morogoro

 KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia Mfumo wa Bima ya Afya, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekutana na waratibu wake kutoka halmashauri zote nchini kwa lengo la kujipanga kuwafikia wananchi wengi zaidi pamoja na uboreshaji wa huduma kwa wanachama. 

Akifungua kikao kazi hicho cha siku mbili, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema kuwa ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Serikali ya Viwanda ni lazima Mfuko kwa kushirikiana na wadau wake kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa kwa kujiunga na Mfuko ili kuwa na uhakika wa huduma za matibabu. 

“Ili kufikia lengo la Nchi ya Viwanda ambalo Rais wetu amelianzisha, ni lazima tuhakikishe wananchi wote wanakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wanapopatwa na magonjwa na ndio maana tumeamua kabisa tukutane kwa pamoja ili tukubaliane namna bora ya kuwafikia lakini pia kuboresha na kuimarisha huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma,” alisema Bw. Konga. 

Kikao hicho pia kina lengo la kupata mrejesho wa pande zote mbili kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanyika ndani ya Mfuko na kujadili kwa pamoja mambo yanayohitaji kuboreshwa kwa lengo la kuongeza wigo na kutoa huduma bora. Mkurugenzi Mkuu pia alisisitiza juu ya kukabiliana na tatizo la udanganyifu ambalo limekuwa likifanywa na baadhi ya watoa huduma wasiokuwa waaminifu hali inayorudisha nyuma jitihada kubwa za Mfuko za kuimarisha Mfuko. 

Alisema kuwa kwa upande wa Mfuko, umeanzisha mifumo mbalimbali ya TEHAMA ambayo inatumika katika kubana mianya ya udanganyifu kwenye utumiaji wa huduma na uwasilishaji wa madai ya watoa huduma hivyo akawaomba waratibu hao kutoa ushirikiano mkubwa katika suala hili kwa lengo la kulinda uhai wa Mfuko. 

Kwa upande wa waratibu wamesema kuwa mkutano huo ni fursa kubwa kwao kupata taarifa mbalimbali za maboresho yaliyofanywa na kujengeana uwezo wa ushawishi kwa wananchi kujiunga na huduma za Mfuko.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Bernad Konga akifungua kikao kazi kilichohusisha Waratibu wa Mfuko kutoka Halmashauri zote nchini mjini Morogoro.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw. Bernard Konga akifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa katikati ni Meneja wa NHIF, Mkoa wa Morogoro Bi. Agnes Chaki na Kushoto ni Mkurugenzi wa 
Utawala na Rasilimali Watu Bw. Charles Lengeju.
 Waratibu wa Mfuko wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wawezeshaji



Hivyo makala NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake

yaani makala yote NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/nhif-waratibu-wajadili-uboreshaji-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake"

Post a Comment

Loading...