Loading...
title : RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI
link : RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI
RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
RAIS Dk.John Magufuli amesema mtumishi yoyote wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto atakayecheleweshwa dawa na vifaa tiba kutoka bandarini atamchukulia hatua mara moja.
Ametoa kauli hiyo kutokana na taarifa alizonazo kuwa kuna ucheleweshaji wa dawa zinapofika bandarini na hivyo akatoa msimamo wake asisikie dawa zinachelewa kutolewa na iwapo ucheleweshwaji huo unafanywa na waliokuwa wizarani hapo basi ni vilaza.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa akizindua magari mapya 181 yaliyotolewa msaada na Global Fund kwa Bohari ya Dawa(MSD),ili yatumike kusambaza dawa, Rais amesema hataki kusikia tena kuwa dawa zinapofika bandarini zinacheleweshwa.Amesema hatasita kuchukua hatua kwa yoyote ambaye atabainika kuhusika a kukwamisha kwani upo uwezekano wa kukwamishwa kwa dawa za Serikali halafu nyingine za watu binafsi zikatolewa kwa wakati.
Wakati anazungumzia suala hilo la ucheleweshwaji wa dawa bandarini alihoji kama wanaotoa kibali ni Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA) au laa.Hata hivyo akaelezwa jukumu hilo lipo chini ya Wizara ya Afya.Amewaambia viongozi wa Wizara hiyo dawa zinapoingia bandarini zitolewe haraka ili ziende kutumiwa na watanzania kuokoa maisha yao kwani kuna uwezekano wakati dawa zinacheleweshwa bandarini kuna wagonjwa wanapoteza maisha kwa kukosa dawa.
Pia akafafanua au kama wizarani watashindwa kumchukulia hatua anayekwamishwa dawa kutoka kwa wakatai bandarini basi atakachokifanya ni kuwatumbua wote walioshindwa kuchukua hatua na yule ambaye anakwamisha atampa nafasi.
"Kama kuna mtu anakwamisha dawa zisitolewe kwa wakati na wote mliokuwa wizarani mnatii maana yake ni kwamba huyo anayekwamisha ana nguvu kuliko ninyi."Hivyo nitampa nafasi yeye na ninyi nitawaondoa.Wala siwatishii lakini niwaambie ukweli sitaki kusikia habari ya dawa kuchelewa tena bandarini,"amesema Rais Magufuli.
Pia Rais Magufuli amesema kuwa wakati anaingia madarakani moja ya eneo ambalo lilikuwa ni changamoto ni uhaba wa dawa lakini anafurahi kuona hali kwa sasa iko vizuri na ametoa kipaumbele kwa wizara ya afya kwani ni moya wizara ambayo bajeti yake inatengewe fedha nyingi.
Hivyo makala RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI
yaani makala yote RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/rais-magufuliole-wao-watakaochelewesha.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI:OLE WAO WATAKAOCHELEWESHA DAWA ,VIFAA TIBA BANDARINI"
Post a Comment