Loading...
title : WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU
link : WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU
WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU
Na Ripota Wetu,Tanganyika
SHILINGI zaidi ya milioni 152 zimetolewa na wadau wa elimu wilayani Tanganyika,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mhuga akihutubia wadau wa elimu pamoja na mambo mengine walikutana kwa ajili ya kuchangishana fedha hizo wenye lengo la kusaidia maendeleo ya elimu kwa shule za msingi na sekondari.
Meja Jenerali Mstaafu Muhaga ambaye aliyekiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imefanyika Mpanda Mjini,ametoa mwito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuleta maendeleo.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tangayika Salehe Muhando amesema michango yote iliyopatikana lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mhando ameonya mara kadhaa kuhusu uadilifu katika matumizi ya fedha za umma akifafanua maendeleo hayawezi kuja kama ndoto tu bali uthabiti katika katika kutenda na usimamiaji.Pia Mhando akizungumza mbele ya wadau wa Elimu katika ukumbi wa Idala ya Maji mkoani Katavi amewahakikishia kuwa michango ambayo imetolewa itasimamia wa vema na kutumika kwenye malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mbunge wa Jmbo la Mpanda vijijini Suleimani Kakoso ameachangia komputa kwa shule za sekondari,vifaa vya ujenzi na fedha taslimu, nakuzishauri halmashauri mkoani Katavi kuwashirikisha wadau wa maendeleo walioko ndani na nje ya halmashauri zao ili washiriki kuleta maendeleo katika elimu na nyanja mbali mbali.
Wadau wa elimu ambao wameshiriki wanatoka taasisi za kifedha,wafanyabiashara,madiwani halmashauri ya wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara wilayani Tanganyika,wakulima, pamoja na watu binafsi.
Baadhi ya vitu vilivyochangwa na wadau hao mbali ya fedha ni kompyuta 24 zenye thamani ya Sh.milioni 48,mifuko ya saruji 2281 yenye thamani ya Sh.milioni 41,058,000,vitanda dabodeka 25 vyenye thamani ya Sh. 5,000,000
Malumalu box 200 yenye thamani ya Sh.milioni 5 na
Bando za bati 1530 zenye thamani ya Sh.30,400,000.
Pia fedha taslimu Sh.400,000,fedha za ahadi Sh.milioni 17.4,kokoto kubwa tani 14 zenye thamani ya Sh.520,000 na Kokoto Vumbi tan 14 ambazo thamani yake ni Sh.160,000.Mpango huu unatarajiwa kuleta tija kwa ustawi wa elimu katika wilaya hiyo yenye takribani kata 15.
Mkuu wa Wilaya ya Tangayika Salehe Muhando
Hivyo makala WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU
yaani makala yote WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/wadau-wa-elimu-tanganyika-wachanga-mil.html
0 Response to "WADAU WA ELIMU TANGANYIKA WACHANGA MIL 152/- KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU"
Post a Comment