Loading...
title : Waziri wa ulinzi wa Israel atembelea JKCI
link : Waziri wa ulinzi wa Israel atembelea JKCI
Waziri wa ulinzi wa Israel atembelea JKCI

Waziri wa ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman akimpa zawadi mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akishuhudia. Tangu mwaka 2015 JKCI kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto na wazazi wao ambao walifanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Mhe. Liberman alitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel ambao kwa kushirikiana wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo bila malipo .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimpa zawadi ya kitenge Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman alitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel ambao kwa kushirikiana wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo bila malipo.
Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo wa matibabu ya moyo kwa watoto, kusomesha madaktari na wauguzi kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Liberman wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari pamoja na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao walisoma nchini Israel kwa udhamini wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini humo. Picha na JKCI
Hivyo makala Waziri wa ulinzi wa Israel atembelea JKCI
yaani makala yote Waziri wa ulinzi wa Israel atembelea JKCI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa ulinzi wa Israel atembelea JKCI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/waziri-wa-ulinzi-wa-israel-atembelea.html
0 Response to "Waziri wa ulinzi wa Israel atembelea JKCI"
Post a Comment