Loading...

Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania

Loading...
Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania
link : Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania

soma pia


Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania

Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda akiongea baada ya Airtel kuibuka kinara katika kutoa hudumia kupitia mitandao ya kijamii, akishuhudia Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Bi Bearice Singano Mallya.
------------------------------------
Airtel Tanzania imetajwa kuwa moja ya makampuni bora ambayo yanajibu vizuri maswali ya mashabiki na wateja wake katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2018.
Ripoti hii imetolewa na kampuni ya Socialbakers ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii. 
Kwa mujibu wa Socialbakers, tathmini ya robo hii ya mwaka ilifanyika kuanzia Januari 1, 2018 hadi Machi 31, 2018 na kuifanya Airtel Tanzania iibuke kidedea.
Kampuni hiyo ya Social bakers imekabidhi cheti kama ishara ya ushindi huu na kuonesha kuwa Airtel iliweza kujibu vizuri maswali ya mashabiki wake na wateja kupitia mtandao wa Face book kwa asilimia 98 na hivi kuyapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania. 
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda alisema wanajivunia kupata utambulizi huo na inaonesha jinsi gani wamekuwa wakijituma kuhakikisha wateja wao wanapata majibu ya maswali yao kwa wakati kupitia mitandao ya kijamii hususani Face book. 
“Tunayo faraja kuweza kutambuliwa kwa namna hii na sisi tunalo jukumu la kuendelea kuhakikisha wateja na mashabiki wetu wanapata majibu wanayohitaji kwa wakati na mitandao ya kijamii imeturahisishia kazi hii hususani kupitia Face book tumeweza kujibu maswali kwa haraka na kwa wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema. 
Mitandao ya kijamii kama Face book inatakiwa kutangazwa zaidi ili itumike kwa wingi kwani itapunguza usumbufu wa wateja kusubiri majibu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa hapo awali ambapo walilazimika kupiga simu Airtel. “Kwa kupitia mitandao ya kijamii majibu yanatolewa hapo hapo na hili ndilo limetufanya tutambuliwe kwani tumeweza kutumia njia hii kwa ufanisi mkubwa na tathmini ya Socialbakers imeonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu tulijibu maswali kwa asilimia 98 na hivi kuibuka kidedea,” aliongeza Ndunda
Kwa mujibu wa Socialbakers, utambulizi huu unatokana na namna kampuni imeweza kujibu maswali ya watu kwa muda wa mwezi mitatu. Ili utambuliwe, lazima kampuniipokee maswali 50 kutoka kwa mashabiki katika robo husika na maswali hayo yaweze kujibiwa kwa zaidi ya asilimia 65. 
Socialbakers ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii hususani Face book, Twitter, Google+, LinkedIn na YouTube ili kusaidia makampuni kujua mafanikio ya kampeni mbalimbali kupitia mitandao hii.  


Hivyo makala Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania

yaani makala yote Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/airtel-tanzania-yaongoza-katika.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania"

Post a Comment

Loading...