Loading...

ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE

Loading...
ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE
link : ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE

soma pia


ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE

NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA

ASKOFU Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Magharibi Tabora Isaac Laise amesewma Watanzania wanatakiwa kutoruhusu mataifa ya nje yawagawanye kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Alisema kuna baadhi ya mataifa makubwa yanaweza kutaka kupenyeza ajenda zao ili kujinufaisha kisiasa au kiuchumi na kuiacha Tanzania ikiwa imegawanyika kama wananchi hawatakuwa makini kulinda umoja wao.

Askofu Laise alisema hayo hivi karibuni mjini Tabora wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la ulinzi na usalama lilioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na kuwashilikisha wadau mbalimbali.

Alisema jamii ya Watanzania inapaswa kuwa waangalifu na mataifa makubwa ambayo yanakuwa na ajenda zao binafisi na zinaposhindwa kufanikiwa wanaweza kuwa kuwagawanya kwa misingi ya udini, ukabila hata itikadi ya kisiasa ili kuhakikisha wanachohitaji wanakipata.

“Tusiruhusu maadui wa nje watugawanye kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa au kiuchumi ambayo wakati mwingine yako kwa ajili ya kutaka kunyonya rasilimali hapo nchini…jambo la msingi ni kuendelewa kulinda umoja wetu, amani na utulivu tulijaliwa na Mwenyezi Mungu” alisema Askofu huyo.

Alisema kila Mtanzania anapaswa kuwa mdau mkubwa wa amani ya nchi hii kwa kuiilinda na kuitunza ili hatimaye iweze kumsaidia katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo yake na Taifa kwa ujumla.

Aidha Askofu Laise alisema kila mwananchi katika nafasi ni lazima atende haki na kusiwepo na vitendo ambavyo vinalazimisha haki kununuliwa

Alisema jamii ya Watanzania inapaswa kuwa waangalifu katika nyakati hizo ambapo Serikali inapambana na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijinufaisha na rasimali za taifa kwa maslahi yao kutumiwa na mataifa makubwa kuwagawanya kwa misingi ya udini, ukabila hata itikadi ya kisiasa.


Hivyo makala ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE

yaani makala yote ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/askofu-laise-watanzania-msikubali.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ASKOFU LAISE: WATANZANIA MSIKUBALI KUGAWANYWA NA MATAIFA YA NJE"

Post a Comment

Loading...