Loading...
title : BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA
link : BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA
BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUTANO wa Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na China unatarajia kuanza kufanyika Beijing nchini China.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Remidius Emmanuel kutoka Beijing,China amesema kesho Aprili mwaka huu saa saba mchana (saa za China ) kutakuwa na mkutano huo.
Lengo mahususi la mkutano ni kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda na hasa kwenye viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba.
Mkutano huu umeandaliwa kwa pamoja kati ya ubalozi wa Tanzania na Taasisi ya maendeleo ya China na Afrika ( China- Africa Development Fund) ambayo iko chini ya Serikali ya China na ni sehemu ya mwitikio wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ya kuona tunavutia uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya dawa ili nchi yetu iweze kuzalisha kwa ajili ya soko la ndani.
"Kwa hiyo tumeitisha mkutano huu na kuna mwitikio mkubwa na kuna kampuni kama 20 ambayo yanatengeneza dawa, kampuni kubwa ya hapa China yameitikia mwaliko, yatashiriki kesho ili kuweza kusikiliza fursa ambazo Tanzania inazo katika uwekezaji.
"Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu, utaongozwa na mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhammad Bakari ambaye ataambatana na timu ya viongozi wa sekta ya afya wa Tanzania kutoka taasisi za hospitali ya Taifa ya Muhimbili na taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Chuo kikuu cha Afya cha Mhimbili,mwakilishi kutoka taasisi ya MOI (Muhimbili Orthopaedic Institute)
" Vilevile tutakuwepo ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali kwa wawekezaji hao. Ujumbe huu utakuwepo hapa Beijing kuanzia leo hadi Aprili 12 mwaka 2018,"amesema.
Ameongeza kengo lao ni ifikapo Mei,2018 waandae ziara ya wawekezaji ambao wataonyesha nia sasa yakuja Tanzania kwa ajili ya fursa hiyo ili wakutane na wadau mbalimbali nyumbani nchini Tanzania.
Baadhi ya wadau ni taasisi za uwekezaji TIC,EPZA,ZIPA na wengineo pamoja na taasisi ya MSD.
Amesema mbali na mkutano huo wa jukwaa la biashara, watakuwa na ajenda nyingine mahususi za kujenga ushirikiano kati ya taasisi zao na taasisi za hapa China, matarajio ni kwamba Jumanne ya Aprili 10 mwaka huo ujumbe huu utakutana na na uongozi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha hapa China.
Hivyo makala BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA
yaani makala yote BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/balozi-kairuki-azungumzia-mkutano.html
0 Response to "BALOZI KAIRUKI, AZUNGUMZIA MKUTANO JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA"
Post a Comment