Loading...

Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka

Loading...
Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka
link : Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka

soma pia


Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Maithripala SIRISENA.

Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza, kuimarisha na kukuza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Sri Lanka ambao ulianza mnamo miaka ya tisini. Wakati huo, Sri Lanka ilikuwa inawakilishwa nchini Tanzania kupitia Ubalozi wake wa mjini Kampala, Uganda ambao baadaye ulifungwa na Tanzania ikiwakilishwa nchini Sri Lanka kupitia Ubalozi wake wa New Delhi. Kwa sasa Sri Lanka inakusudia kumteua Balozi wake mjini Nairobi ambaye pia ataiwakilisha nchi hiyo nchini Tanzania.

Katika hafla hiyo, Balozi Luvanda aliambatana na Mwambata Jeshi wa Tanzania nchini India, Col.Amri Salim MWAMI. Aidha, Balozi Luvanda alifanya mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Sri Lanka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Afrika, ambapo ameahidi kushirikiana kwa karibu na watendaji hao katika kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili na ambao utazinufaisha zaidi, hususan katika kuhakikisha uhaulishaji wa uzoefu, teknolojia na utaalam wa Sri Lanka kwa Tanzania kwenye sekta ya viwanda vya nguo, madini na vito mbali mbali na kilimo.

Sri Lanka ni nchi yenye uchumi unaoendelea ingawa imepitia kipindi kigumu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa takriban miaka 25, vita ambavyo vilimalizika mwaka 2009.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Maithripala SIRISENA, Rais wa nchi hiyo
Balozi Luvanda akisalimiana na maafisa waandanizi wa Ikulu ya Sri Lanka
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Maithripala SIRISENA.


Hivyo makala Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka

yaani makala yote Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/balozi-luvanda-awasilisha-hati-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka"

Post a Comment

Loading...