Loading...
title : BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI
link : BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI
BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI
BONDIA Idd Mkwera amesaini mkataba wa kuzipiga na bondia machachari Ramadhani Shauri katika mpambano wa raundi 10 utakaofanyika Mei 5 mwaka huu Uwanja wa Ndani wa Taifa.
Mkwera amesaini mkataba huo ikiwa ni siku chache zimepita tangu apoteza mpambano wake wa nje uliofanyika Riga Ratvia kwa point. Akizungumza wakati wa utaiaji saini huo leo, Mkwera amesema yeye anachojua ngumi ndio kazi yake,hivyo kwake kazi ni kazi tu na haijalishi anacheza na nani. Hivyo amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kwenda kushudia mpambano huo.
Akijibu mapigo Shauri amesema wapenzi wangu na mashabiki zangu wamemikosa tangu mwaka jana alivyopoteza pointi katika uwanja ule ule. "Sasa nilitoka kidogo nje ya Tanzania hivyo nimerudi na kasi mpya nguvu mpya njoeni mshuhudie ngumi zinavyopigwa," amesema.
Kwa upande wa Promota wa mchezo huo Evalist Ernest amesisitiza kuwa mabondia hao watacheza mpambano wa raundi 10 katika uzito wa kg 62.5. "Hivyo mje mshuhudie masumbwi siku hiyo mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi kwa vijana tulio wasainisha," ameongeza
Hivyo siku hiyo bondia Haidari Mchanjo atazichapa na Amani Bariki 'Manny Chuga' wakati Karimu Ramadhani atakumbana na Jerms Kibazange na Said Chini ataoneshana umwamba na Hamza Mchanjo. Mapambano hayo na mengine yote yatakuwa wakisindikiza pambano kuu kati ya Idd Mkwera na Ramadhani Shauri watakaozipiga Raundi kumi
Pia watatumia siku hiyo kuuza DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani.
Promota wa mpambano wa ngumi, Evalist Ernest katikati akiwainua mikono juu mabondia Iddi Mkwera (kushoto) na Ramadhani Shauri (kulia) mara baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Mei 5 katika ukumbi wa Uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi. Picha na SUPER D BOXING NEWS
Hivyo makala BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI
yaani makala yote BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/bondia-mkwere-asaini-mkataba-wa.html
0 Response to "BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI"
Post a Comment