Loading...
title : CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA
link : CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA
CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kimesema Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe(ACT-Wazalendo) ni mpotoshaji mkubwa na vyombo vya kisheria vinastahili kumchukulia hatua.
Kimesema Ziito kupotosha kuwa kuna fedha Sh.Trilioni 1.5 za Serikali zimeibiwa si kweli na kwamba wameipitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) hakuna fedha ambayo imepota au kuibiwa na kiasi ambacho kimetajwa kwenye ripoti cha makusanyo na matumizi kipo sahihi .
"Tumepitia kwa usahihi taarifa ya CAG na kujiridhisha hakuna fedha iliyobwa kama Zitto anavyopotosha na kutaka kuaaminisha umma.Huu ni upotoshaji mkubwa na lazima tuukemee maana unaleta sintofahamu kwenye jamii."Zitto siku hizi amekuwa na tabia ya uongo.Nimetoa tafsiri yangu na kuelezea ukweli kuhusu fedha hizo anazodai kuwa hazipo.CCM hatuwezi kukaa kimya wakati kuna muongo mmoja anafanya kazi ya kupotosha na kuaminisha umma kitu ambacho si cha kweli,"amsema Polepole.
Amefafanua taarifa ya CAG kuwekwa wazi ni msimamo wa Serikali na hawana tatizo na kuongeza kwa bahati mbaya kuna utamaduni wa baadhi ya watu kila jambo la Serikali hata liwe nzuri wao lazima walififishwe Pia amekiri Serikali ya CCM imeanza kuchukua hatua kwa kuwawajibisha waliosababisha ufujaji wa fedha za umma na mtindo huo uendelee na mtu akibainika mkosaji achukuliwe hatua .
"Mkaguzi amefanya ukaguzi na kubaini kuna maeneo yanaviashiria vya ubadhirifu hatua zimechukuliwa.Uongozi wa awamu ya tano unajinasibu kwa uongozi bora ambao umejikita kwenye kufanya kazi na haupo tayari kuona ubadhirifu unafumbiwa macho uwe ndani ya Serikali, kwa taasisi za umma au binafsi na hata kwenye vyama vya siasa"amesema.
Amesema ni utaratibu mzuri na ndio maana yote ambayo CAG ameona wamekubaliana yafanyiwe kazi na kusisitiza wanafahamu Zitto amelelewa vibaya huko nyuma lakini anatakiwa kufahamu sasa ni Serikali ya Awamu ya Tano na CCM ni mpya haipo tayari kuwavumilia wapotoshaji.
"Zitto amekuwa na tabia ya uongo uongo sana, siku za nyuma alianza kuongopa kuhusu njaa wakati njaa hakuna na anaongopa kuhusu ripoti ya CAG.Vyombo vya kisheria vimchukulie hatua maana kuongopa ndani ya nchi yetu ni kosa,"amesisitiza.
Hivyo makala CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA
yaani makala yote CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/ccm-waamua-kumjibu-zitto-kuhusu-tril-15.html
0 Response to "CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA"
Post a Comment