Loading...
title : Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam
link : Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam
Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Taasisi ya Tulia Trust imezindua Tulia Marathon itakayofanyika Mei 6 katika uwanja Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa Tulia Marathon, Mratibu wa mashindano hayo na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema kuwa mashindano ya mbio hizo kwa fedha zitakazopatikana ni kwa ajili ya afya hususan afya ya mtoto kwa jamii ya Mbeya.
Dk. Tulia amesema kuwa amekuwa anaungwa mkono na wadhamini katika kufanikisha taasisi hiyo kuendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali katika kuandaa michezo.Amesema kuwa mashindano ya mbio hizo yatakuwa na muonekano tofauti na mengine yaliyowahi kufanyika nchini kutokana na kujumuisha kila kundi katika jamii.
Aidha amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa ya kilomita 42 Full , Half Marathon 21 , wanafunzi kwa mbio za kilomita Tano , mbio za baiskeli kilomita 150 kwa wanaume na kilomita 75 kwa wanawake, Kilomita tano watakimbia watu kwa ajili ya kujifurahisga pamoja na watoto watakimbia kilomota mbili.
Fomu kwa ajili ya maombi ya kushirikia mashindano ya Tulia Marathon zinapatikana katika tovuti yawww.tuliatrust.org
Wadhamini wa mashindano ya Tulia Marathon hayo ni Mo Dewj Foundation, Mantra Tanzania, Tatu Muzuka pamoja na Derm Electrics T LTD.
01.Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uzinduzi wa Tulia Marathon itakayofanyika Mbeya, leo jijini Dar es Salaam.
02. Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga akizungumza kuhusiana na kudhamini mashindano ya Tulia Marathon
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akimkabidhi tshirt, Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga kwa kutambua mchango wa Tatu Muzuka katika kudhamini mashindano hayo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam
yaani makala yote Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/dktulia-azindua-tulia-marathon-jijini.html
0 Response to "Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam"
Post a Comment