Loading...
title : DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20)
link : DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20)
DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20)
CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimetangaza kozi ya siku tano 5 ya waamuzi wa soka iliyoandaliwa mmahsusi kwa ajili ya vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Akizungumza leo Ofisa Habari wa DRFA Karim Boimanda amesema kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) na Chama cha waamuzi itawahusu zaidi vijana waliochini ya umri wa miaka 20.
Amesema kozi hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa programu ya maendeleo ya soka la vijana (Youth Development Program) ambayo ilianza kwa kozi ya ukocha wa soka la vijana iliyomalizika mwanzoni mwa Machi.
Ametaja ada ya ushiriki wa kozi hiyo inayotarajiwa kuanza Aprili 30 mwaka huu ni Sh.25000 huku msisitizo wakati wa usajili ukitarajiwa kuwekwa kwenye suala la umri.
Kozi hiyo itafanyika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume jijini Dar es Salaam na malipo yote yanatakiwa kufanyika kupitia benki ya Akiba Commercial (ACB) kwenye akaunti namba 10100548227 (DSM REGIONAL FOOTBALL ASSOCIATION) kisha kuwasilisha 'deposit slip' kwenye ofisi za DRFA kwa ajili ya kukabidhiwa risiti.
Hivyo makala DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20)
yaani makala yote DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/drfa-kuendesha-kozi-ya-waamuzi-vijana-u_17.html
0 Response to "DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20)"
Post a Comment