Loading...
title : HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM
link : HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM
HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa utekelezaji wa Ilani wa chama cha Mapinduzi na kusema kuwa ameiona thamani ya fedha katika miradi yote aliyoitembelea hivyo mshikamano uliopo uendelezwe.
Amayezungumza hayo jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi aliyoifanya Manispaaa ya Kigamboni yenye lengo la kuona ni naman gani Ilani ya Chama inatekelezwa.
Akizungumza na watumishi na wananchi wanao shiriki kusimamia miradi Bi.Kamba amesema kuwa, Miradi yote inatekelezwa katika ubora na ndani ya wakati na thamani ya fedha ( Value for money) inaonekana.
"Miradi yenu mizuri na inatekelezwa kwa ubora na wakati, mnaspidi nzuri sana hii inaonesha ni naman gani mnaushirikiano, Kigamboni ni Wilaya changa lakini mambo mnayofanya mnawazidi hata Wilaya kongwe, tumependa" Alisema Kamba
Aliongeza kuwa ameona ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba jamii imeshiriki kikamilifu hali inayopelekea kuona wanao wajibu wa kutunza na kusimamia miradi yao ndio maana wameweza hata kufikia makubaliano ya kuomba punguzo la bei ya ununuzi wa vifaa vinayohitajika kwenye ujenzi miradi.
Aidha Bi. Kamba alisema kuwa sheria ya manunuzi inagharimu sana utekelezaji wa miradi , urasimu mwingi tofauti na utaratibu wa local fundi unaosaidia kutumia fedha kidogo na miradi kujengwa kwa wakati huku thamani ya fedha ikionekana. Kamba aliwataka watumishi kuona anao wajibu na sehemu yake ya kufanya kazi na kuhudumia wnanchi ikiwa ni utekelezaji wa ilanai na kuhakikisha lengo lililowekwa linafikiwa kwa kiwango cha juu. ![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXi8e_RpqND4R5x5ObhnylCT0A2SWqw7JchmXx4I8j9Em9Kh4AJRiEwuU-HQix5kqexaOAEHocUE3qi_J-IFthkdDo_k3ZC_BYyvK0uihaT8VWmbqBlM-owr6jbZP7NIHHFv_9cL02mK6k/s640/DSC_0796.JPG)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bi. Kate Kamba akizungumza na kutoa pongezi zake kwa Manispaa ya Kigamboni.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIgTExk11juuL094kDJTrvfMWu03akYDXn0XDHpms3oKlEpEOakjTR0IFzlpMZJ2QJ7WruRvmdeHazYLWO68Qk8IDsOlC15Uuf2IiWgPvHLcpfFNXQpnJy8UedENqh8gela5joyNGdQeK0/s640/DSC_0733.JPG)
Baadhi ya Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa alipokuwa akizungumza nao
Baadhi ya Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa alipokuwa akizungumza nao
jengo la wamama wajawazito likiwa kwenye hatua ya renta
Jengo la maabara na upasuaji likiwa katika hatua ya upauaji kama inayoonekana katika picha
muonekano wa jengo la kuhifadhia maiti.
Hivyo makala HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM
yaani makala yote HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/halmashauri-manispaa-kigamboni.html
0 Response to "HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM"
Post a Comment