Loading...
title : Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8
link : Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8
Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8
Na Bahati Mollel-TAA, Iringa
TIMU ya Ofisi ya Rais Ikulu imewachapa bila huruma wenyeji RAS Iringa kwa kuwafunga magoli 49-8 katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) mkoani Iringa.
Ikulu inayofundishwa na kocha mzoefu Mary Protas ambapo wafungaji wake Fatuma Machenga aliibeba timu yake kwa kufunga magoli 48 huku Irene Elias alifunga bao moja pekee. Magoli ya RAS Iringa yamefungwa na Warda Sapal na Zitaamanzia Kididi kila mmoja manne.
Katika mchezo wa soka timu ya RAS Iringa ilifungwa na Tumbaku ya Morogoro kwa magoli 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja w Samora.
Washindi walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Ramadhani Shegodo aliyefunga dakika ya tisa baada ya kupata pasi kutoka kwa Mohamed Mtawal; huku bao la pili lilipatikana dakika ya 29 kwa shuti kali la Ushindi Nzogela.
Bao la tatu lilifungwa na Salum Idd katika dakika 52 baada ya kupiga krosi murua iliyomshinda kipa Mashaka Peter aliyejikuta akiusindikiza mpira langoni mwake.
Hatahivyo, Tumbaku itabidi wajilaumu kwa kukosa magoli mengi ya wazi, ikiwemo dakika ya 20 mshambuliaji wake Issa Simbaliana kukosa penalti iliyotolewa na mwamuzi Steven Makuka baada ya Nzogele kuchezewa rafu na Dickson Kiboye wa RAS Iringa, lakini kwa kupaisha mpira juu ya goli.
Mfungaji Fatuma Machenga (GS) wa Ikulu akifunga mbele ya mlinzi wa RAS Iringa (GK), Maria Mwita katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) Iringa. Ikulu wameshinda magoli 49-8.
Mlinzi wa pembeni Ester Turuka (WA) wa RAS Iringa akirusha mpira kwa mfungaji wao Warda Sapal (GS) huku mlinzi Lilian Sylidion (GD) wa Ikulu akijitahidi kuzuia katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) Iringa. Ikulu wameshinda magoli 49-8.
Mchezaji Sharifa Hamis (kulia) akifanya mazoezi ya kucheza bao na Ambakisye Mwasunga (kushoto) wakifanya mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Mei Mosi kwa upande wa michezo ya jadi inayofanyika kwenye uwanja wa Somora mkoani Iringa. Katikati ni mchezaji wa mchezo wa draft Bw. Omar Said akiangalia.
Beki Nestory Tweve (3) wa timu ya Tumbaku ya Morogoro akitafuta njia ya kuwapita Francis Singa na Abdul Kawamba (wenye jezi nyeusi) wa RAS Iringa, katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora. Tumbaku walishinda magoli 3-0.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8
yaani makala yote Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/ikulu-yaiadhibu-ras-iringa-kwa_18.html
0 Response to "Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8"
Post a Comment