Loading...

MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA.

Loading...
MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA.
link : MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA.

soma pia


MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA.


Image result for icha ya majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wajiepushe na tabia ya kuingiza siasa katika suala la kuwaondoa wananchi waishio mabondeni  kwa kuwa jambo hilo linafanywa kwa maslahi ya wananchi wenyewe.

Amesema wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha na mali zao kila yanapotokea mafuriko, hivyo ni vizuri kwa viongozi wakiwemo wabunge washirikiane na Serikali kuwahamasisha wakazi wote wa mabondeni wahame.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Aprili  19, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Temeke, Bw. Abdallah Mtolea katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

 “Mara nyingi Serikali imekuwa ikiwataka wakazi ya maeneo ya mabondeni kuhama  ila suala hilo limekuwa likikwamishwa na masuala ya kisiasa. “Wabunge ni mashahidi jambo hili linapoamuliwa, zinaingizwa siasa.”

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wananchi walioathiriwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko zikiwemo familia za watu 12 waliofariki mkoani Dar es Salaam.

Katika swali lake, Bw Mtolea alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kudhibiti madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dar es Salaam.

Mapema akijibu swali la Mbunge wa Nyang’hwale , Bw. Hussein Nassoro Waziri Mkuu alisema suala la kurejesha miundombinu iliyoharibika linashughulikiwa na kamati za maafa za mikoa na wilaya ambazo kwa sasa zinafanya tathmini ili kujua kiwango cha uharibifu na hatua gani zichukuliwe.

Bw. Nassoro alitaka kujua Serikali imejipangaje katika kurejesha miundombinu iliyoharibika kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito wa wananchi kuhakikisha wanatumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbalimbali ya biashara na chakula. Kuhusu mazao ya biashara amesema Serikali itawasaidia kutafuta masoko.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Bi. Aida Khenani (Viti Maalumu), aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kuandaa masoko ya uhakika kwa mazao ya wakulima.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, APRILI 19, 2018.


Hivyo makala MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA.

yaani makala yote MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/msiingize-siasa-suala-la-mabondeni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA."

Post a Comment

Loading...