Loading...
title : Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini
link : Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini
Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania imezidi kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za intaneti nchini baada ya kuwazawadia wateja wake 676 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.
Katika promosheni hii murwa ambapo Tigo inatoa jumla ya simu janja 12 kila siku, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter.
‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo,’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza katika hafla kama hiyo iliyofanyika mjini Morogoro leo, Mtalaam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) na Mtalaam wa Bidhaa wa Tigo, Jacqueline Nnunduma (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi za simu janja aina ya Tecno R6 kwa washindi wa promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Gladness Mori (alieyeketi) zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Diana Pumpuni (wa pili kushoto) zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Charles Shabani zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini
yaani makala yote Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/promosheni-ya-tigo-yaongeza-matumizi-ya.html
0 Response to "Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini"
Post a Comment