Loading...

Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

Loading...
Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini
link : Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

soma pia


Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanzia tarehe 17 Aprili, 2018.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mhe. Rais Magufuli amewateua Makamishna wa Tume ya Madini kama ifuatavyo:
  1. Bw. Doto James – Katibu Mkuu, Fedha na Mipango.
  2. Bi. Dorothy Mwanyika – Katibu Mkuu, Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
  3. Dkt. Florens Turuka – Katibu Mkuu, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  4. Mhandisi Musa Iyombe – Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  5. Bw. Haroun Athuman Kinega – Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini (FEMATA).
  6. Dkt. Evaristo Emmanuel Longopa – Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  7. Prof. Abdulkarim Hamis Mruma – Mkurugenzi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafutaji Madini Tanzania (GST).
  8. Dkt. Athanas Simon Macheyeki – Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Uteuzi wa Balozi Mstaafu Njoolay umeanza tarehe 17 Aprili, 2018.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2018




Hivyo makala Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

yaani makala yote Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/rais-magufuli-amteua-prof-idris-kikula.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini"

Post a Comment

Loading...