Loading...
title : RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMWAGA PONGEZI KWA NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS
link : RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMWAGA PONGEZI KWA NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS
RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMWAGA PONGEZI KWA NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS

Ngorongoro Heroes wamefanikiwa kusonga kwenye raundi ya pili ya kufuzu fainali za Africa za Vijana chini ya miaka 20 zitakazochezwa Niger mwezi Novemba baada ya ushindi wake wa penati 5-6 dhidi ya DR Congo baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Tanzania wakati Serengeti Boys wenyewe wamefuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Vijana ya Cecafa chini ya miaka 17 inayoendelea huko Burundi.
Rais wa TFF Ndugu Karia amesema kufanya vizuri kwa timu hizo za vijana ni faraja kubwa kwa Tanzania na inaonesha namna ambavyo TFF inaendelea kuwekeza kwenye soka la vijana.Amesema Vijana hao wa Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys wameonesha jitihada kubwa na wanastahili pongezi kwa jitihada hizo pamoja na jitihada za mabenchi ya ufundi ya timu hizo.
“Tumepokea matokeo ya Vijana wetu wa Ngorongoro na Serengeti Boys kwa furaha kubwa kwasababu tumekuwa tukihakikisha timu hizi zinapata maandalizi mazuri ambayo yanaonekana uwanjani kwa kupata matokeo mazuri ambayo yanailetea sifa kubwa Tanzania kwa ujumla” alisema Karia.
Aidha Rais wa TFF Ndugu Karia amesema TFF itaendelea na jitihada kuzipatia maandalizi mazuri zaidi timu hizo ili ziweze kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayowakabili.
Amesema TFF inajivunia vijana hao ambao wanaonesha mwanga mkubwa na amewaomba watu mbalimbali,Taasisi,makampuni kuunga mkono jitihada za TFF na kuiga mfano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro waliojitokeza na kuisaidia Ngorongoro Heroes katika safari yake ya kwenda DR Congo kwenye mchezo wa marudiano.
Amemalizia kwa kuwashukuru wote wanaounga mkono jitihada za TFF kuendeleza mpira wa Tanzania huku akiishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuunga mkono na ushirikiano wao kwa TFF.
Hivyo makala RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMWAGA PONGEZI KWA NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS
yaani makala yote RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMWAGA PONGEZI KWA NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMWAGA PONGEZI KWA NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/rais-wa-tff-wallace-karia-amwaga.html
0 Response to "RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMWAGA PONGEZI KWA NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS"
Post a Comment