Loading...

TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini

Loading...
TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini
link : TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini

soma pia


TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini

Mkufunzi Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kutoka kitengo cha KEIZAN, Janeth Senkondo (akiwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa za ngozi kwenye mafunzo yanayoratibiwa na TanTrade.

Wazalishaji thelathini (30) wa bidhaa za ngozi kutoka Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania (TALEPPA) wamejengewa uwezo kwa kupewa mafunzo ya siku tatu yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Mafunzo hayo yaliyoongozwa na Bw Emmanuel Miselya, Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara kutoka TanTrade amesema kuwa lengo la kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa za ngozi ni kuwasaidia kuwa na ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

‘’Sekta hii ina rasilimali nyingi na ikitumiwa vizuri kwa kushirikiana na wazalishaji wenyewe Tanzania itakuwa na viwanda vingi vya ngozi na bidhaa zake na wananchi watapata ajira itakayowaongezea kipato kikubwa kwa sababu kuna fursa kubwa ya masoko ndani na nje ya nchi hivyo kuongeza wigo wa kodi”, alisema Bw Miselya.

Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa TanTrade itahakikisha inatoa mafunzo kwa wazalishaji wa bidhaa zenye muelekeo wa viwanda ili rasilimali za nchi zitumike vizuri na kuweza kuvutia ongezeko la uwekezaji nchini.

Nae, Bw Johnson Kiwia, Afisa Viwango kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), amewashauri wazalishaji wa bidhaa za ngozi kuzingatia kutumia malighafi iliyothibitishwa na taasisi hiyo ili kuwapa ujasiri wa kufanya biashara ndani na nje ya nchi na kuweza kumudu ushindani wa soko.

Kwa niaba ya wanufaika wa mafunzo hayo, Bw.Timoth Funto, Katibu wa Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania (TALEPPA) ameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata ujuzi wa masoko yatakayowawezesha kutatua changamoto ya namna ya kusimamia biashara zao ili kukidhi hitaji la msingi lililokuwa linawatatiza katika uzalishaji.

Mafunzo ya awamu ya tatu yamejikita kwenye uzalishaji bora wa bidhaa zenye viwango, kuzingatia usalama mahala pa kazi na namna ya kubuni bidhaa zenye mvuto na kuendana na mitindo ya kisasa yenye kupendwa na watumiaji wengi.

Taasisi zilizoshiriki kuwajengea uwezo wazalishaji hao ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia kitengo cha KAIZEN, TBS, VETA, OSHA na DIT kampasi ya Mwanza.


Hivyo makala TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini

yaani makala yote TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/tantrade-yawapiga-msasa-wazalishaji-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini"

Post a Comment

Loading...