Loading...
title : TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI
link : TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI
TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kocha Msaidizi wa kikosi cha Njombe Mji Mrange Kabange amesema kuwa bado wana nafasi ya kuendelea kusalia ligi kuu hata baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba hapo jana.
Njombe Mji walishindwa kutamba kwenye uwanja wa Sabasaba baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa wekundu wa Msimbazi Simba magoli yote yakifungwa na John Bocco.
Baada ya kipigo hicho, Njombe Mji wamesalia katika nafasi ya 15 wakiwa na alama 18 nyuma ya Majimaji inayoshika mkia.
Kocha huyo amesema kuwa, bado wana michezo nane ambapo kama watafaniliwa kuondoka na ushindi wanauwezo wa kuendelea kusalia katika ligi kuu msimu ujao.
"Bado tuna nafasi kuendelea kusalia ligi kuu msimu ujao, tuna michezo nane ambapo mipango yetu ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mechi hizo na tunaamini tunabaki kwani kikosi changu kina uwezo,"amesema Kabange.
"Kikosi changu kina wachezaji wazuri na wanauwezo wa kukupa matokeo, katika mchezo wa jana hatukuwa vizuri ila mechi zilizobaki tutapambana kufa na kupona kupata matokeo mazuri,"
Njombe Mji ilifanikiwa kupanda ligi kuu msimu wa mwaka 2017/2018 na wameonekana kusuasua hususani raundi ya pili lakini walifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup na kuondolewa na Stand United.
Hivyo makala TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI
yaani makala yote TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/tutasalia-ligi-kuu-msimu-ujao-kocha.html
0 Response to "TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI"
Post a Comment