Loading...

Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini

Loading...
Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini
link : Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini

soma pia


Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini

Na Genofeva Matemu – WHUSM
Wadau wa sekta ya Filamu nchini wameiomba bodi ya filamu kunao umuhimu wa kuongezea makali ya kikikanuni katika kusimamia vibanda vinavyoonyesha sinema nchini kwa kuzifanya kanuni maalumu za kusimamia vibanda vya sinema kuzingatia kumuwajibisha mmiliki wa Eneo au kibanda husika badala ya kumuwajibisha aliyeajiriwa kuendesha vibanda hivyo peke yake.
Hayo yamesema na Afisa Utamaduni Sekretariate ya Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Adorph Halii wakati wa kikao cha maafisa utamaduni wa mkoa wa Dar es Salaam na Bodi ya filamu katika kupitia na kutoa maoni juu ya kanuni maalum za kuendesha vibanda vya kuonyesha filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Aidha Bw. Adorph amezitaka bodi za filamu katika ngazi za mikoa na wilaya kuwa hai ili ziweze kuunganisha nguvu kwa pamoja kusimamia vizuri vibanda vya kuonyeshea sinema kwani wakilegalega katika kusimamia vibanda hivyo kutapelekea mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii hivyo kuwa na taifa lisilo na maadili kutokana na kuwaacha watoto wadogo kuangalia filamu zisizoendana na umri wao.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Bodi ya filamu imekua ikipokea malalamiko mengi sana kuhusu vibanda vinavyoonyesha sinema kuwa vimekua vikisababisha uvunjifu wa maadili katika jamii hivyo kuwataka maafisa utamaduni wa mkoa na wilaya kutoa elimu kwa wamiliki wa vibanda hivyo ili kuweza kuepukana na adhabu zitakazotolewa endapo kanuni hizo zitapita.
 Afisa Utamaduni Sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Adorph Halii (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Dar es Salaam, wilaya zake pamoja na Bodi ya filamu katika kupitia na kutoa maoni juu ya kanuni maalum za kuendesha vibanda vya kuonyesha filamu leo Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akiwaonyesha wajumbe wa kikao cha kupitia na kutoa maoni juu ya kanuni maalum za kuendesha vibanda vya kuonyesha filamu (hawapo pichani) moja ya kitambulisho kitakachotolewa kwa wadau wa sekta ya filamu kutokana na vigezo vilivyowekwa wakati wa kikao na wadau hao leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Utamaduni Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Bw. Emanuel Ndumukwa (katikati) akichangia mada wakati wa kikao cha Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Dar es Salaam, wilaya zake pamoja na Bodi ya filamu katika kupitia na kutoa maoni juu ya kanuni maalum za kuendesha vibanda vya kuonyesha filamu leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Utamaduni Wilaya Kinondoni Bibi. Joyce Kiriho. Picha na Genofeva Matemu - WHUSM

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini

yaani makala yote Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/wadau-wa-sekta-ya-filamu-waomba-kanuni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wadau wa Sekta ya Filamu waomba Kanuni kali za kusimamia vibanda vya kuonyeshea filamu nchini"

Post a Comment

Loading...