Loading...
title : WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA
link : WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA
WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu wamekubali kuunga mkono Serikali katika Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mkoa wa Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi Juni mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa na Wafanyabiashara hao katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa kilichofanyika jana Mjini Bariadi, ambacho kilifanyika kwa lengo la kuzungumzia fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo, changamoto zinazowakabili na utatuzi wake.
Awali akifungua kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imekusudia kuwa na shule kubwa itakayoweza kuchukua wanafunzi 1000 ambayo itakayopatikana kwa kujenga upya shule ya Sekondari Simiyu (Kidato cha kwanza hadi cha Nne), ambapo aliahidi kuwa ofisi yake itatoa fedha kiasi na akawaomba wafanyabiasha wazawa kuchangia Ujenzi wa shule hiyo kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa.
Amesema pamoja na kujenga upya Shule ya Sekondari Simiyu, katika shule hiyo kutajengwa mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike ili wanafunzi wote wa kike wasome wakiwa wanafunzi wa bweni(boarding).
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akizungumza katika kikao cha Wafanyabiashara wa Mkoa huo na Mkuu wa Mkoa huo katika Kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao chao na Mkuu huyo wa Mkoa kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Hivyo makala WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA
yaani makala yote WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/wafanyabiashara-mkoani-simiyu-waunga.html
0 Response to "WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA"
Post a Comment