Loading...
title : WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO
link : WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO
WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
Shirika la Tujenge Tz Innovation limeanzisha mradi kupitia shindano Ubunifu la Tujenge TZ lenye lengo la kuchochea uwezo wa vijana katika kubuni na kuboresha mfumo mzima wa uendeshaji shughuli za ujasiliamali zenye manufaa kwa jamii. Shindano hili litakuwa la wazi na haki kwa wajasiriamali wote vijana watakaoshiriki kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha cha jamii.
Akizungumza leo Mwanzilishi wa mradi huu ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Unleashed Afrika, Khalila Kellz Mbowe ameeleza kuwa mradi huu umenuia kuongeza uwezekano na ukuaji wa kasi wa biashara zinazoendeshwa na vijana hivyo kuzifanya ziwe na wigo mpana wa kunufaisha jamii.
Aidha ameeleza kuwa washindi watapata fursa ya kipekee ya kuhudhuria mafunzo ya kina ya wiki moja ya kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi yao.
Naye Kadele Mabumba Meneja mradi kwa Tanzania na Uganda wa Hanns Foundation amesema Mradi wa Tujenge Tz Innovation Challenge ni wa kukuza shughuli za ujasiriamali wenye kuleta manufaa ya kijamii hasa ujasiriamali hapa Tanzania.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa True Maisha, Erick Chrispin amesema mradi huu unalenga kuongeza ubora wa manufaa ya jamii yanayotokana na shughuli za kijasiriamali katika maeneo yao.
Mradi huu umeanzishwa ili kuchochea uwezo wa vijana katika kubuni na kuboresha mfumo mzima wa uendeshaji shughuli za ujasiriamali zenye manufaa kwa jamii.
Shindano hilo litaendeshwa sambamba na kampuni ya Unleashed Afrika, True Maisha pamoja na shirika la Kijerumani la Hanns Seidel Foundation.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Unleashed Africa, Khalila Mbowe(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano wajasiriamali vijana lililozinduliwa leo kwa ajili ya kuinua vijana kiuchumi hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Julia Berger
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya True Maisha, Erick Chrispin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu watakavyosimamia shindano hilo kwa kutoa mafunzo kwa washindi watakaopatikana mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo lililozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mradi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Kadele Mabumba.
Meneja Mradi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Kadele Mabumba(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyojipanga kutekeleza shindano la wajasiliamali vijana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya True Maisha, Erick Chrispin na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Julia Berger
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Julia Berger akibonyeza kitufe kuashiria ufunguzi wa shindano la wajasilamali vijana kwa mkoa wa Dar es Salaam watakaoshiriki kupitia tovuti ya www.tujengetzchallenge.co.tz.
Hivyo makala WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO
yaani makala yote WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/wajasiriamali-vijana-kuwezeshwa-kupitia.html
0 Response to "WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO"
Post a Comment