Loading...
title : WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA
link : WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA
WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA
![](https://i2.wp.com/ruvumatv.co.tz/wp-content/uploads/2018/04/thumb_553_800x420_0_0_auto.jpg?resize=660%2C400)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue, ameitaka Menejimeti ya Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano wa kusimamia ujengaji wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira.
Chezue amesema hayo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wakati akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo.
“Kuna wakuu wa idara na vitengo wanaingia moja kwa moja kutokana na idara zao msisubiri kuambiwa fanya kitu Fulani jitume na washirikishe waliochini yako ili kufanikisha lengo hili kwani uwanja huo ni wa Halmashauri na si Mkurugenzi pekee yake ”Amesema Chezue.
Aidha Mkurugenzi amesema uwanja huo utakuwa ni chanzo cha mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kutokana na kukodisha Hostel, kukodisha vibanda vya biashara na viingilio vya milangoni. Pia kuinua kipato cha wajasiriamali ambao watapata fursa ya kufanya biashara wakati wa michezo, na jamii itapata fursa ya kuziona timu mbalimbali.
Vilevile amesema lengo la kujenga uwanja huu ni kuibua na kukuza vipaji vya vijana wa Ruangwa kwenye michezo mbalimbali ili kuweza kupata ajira kwani michezo kwa sasa ni ajira. “Uwanja huo utatumika kwa michezo ya kitaifa na kimataifa kwasababu vipimo vyake ni vya kimataifa”Amesema Chezue. Naye Afisa Michezo wa Wilaya Simon Mwambe amesema kwasasa kazi zinaendelea wameishapeleka mchanga kwa ajili ya kufyatua tofali za kujengea ukuta katika uwanja huo.
“Tumeisha chimba msingi wa kujenga ukuta, tuna cement za kutosha na maji yapo tumefunga pampu kwenye kisima kilichochimbwa uwanjani hapo na kesho zoezi la kufyatua tofali litaanza” amesema Mwambe. Hata hivyo Afisa Michezo amesema suala la kuazima vitendea kazi kwa watu binafsi linasababisha kazi zisimame kwa sababu wakati vifaa vinaenda kukodiwa na muhusika anakuwa amekodisha au anatumia kwa shughuli zake.
Hivyo makala WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA
yaani makala yote WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/wakuu-wa-idara-na-vitengo-washiriki.html
0 Response to "WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA"
Post a Comment