Loading...

WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM

Loading...
WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM
link : WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM

soma pia


WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wakazi wawili wa Dar es salaam, wameibuka washindi shindano la shika ndinga lililoendeshwa na kituo cha Radio cha Efm.

Washindi hao ni Ashura Ramadhani mkazi wa Bunju ambaye alipiga simu na kupata nafasi hiyo kupitia kipindi cha uhondo.Mwingine ni Abbas Awadhi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala ambaye alipata nafasi ya kushiriki katika shindano hilo kupitia kipindi cha Genge kinachoendeshwa na radio Efm.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi za Washindi hao Meneja Mkuu wa Radio Efm na Tv E, Dennis Busulwa(Sebo) amesema kuwa washindi hao wameshinda pikipiki na kupatiwa tiketi ya kushiriki fainali za shika ndinga zitakazo fanyika Dar es Salaam mara baada ya kuwapata washindi wa mikoani.

Amesema kuwa siku ya jumatatu washindi hao watafika katika ofisi za Efm na Tv E kwa ajili ya kubadilisha majina ya kadi za pikipiki hizo kutoka jina la kampuni kwenda majina yao.

Washindi hao ambao wamepatikana kupitia mchakato mrefu ulioanza asubuhi kwa mbio za kukimbia na Vikombe vya maji kisha ikaja awamu ya pili ya kukimbia na mayai ambayo iliwapeleka fainali.

Katika hatua ya fainali ya kushika gari ndio iliyotia fora kwa wanawake kuweza kusimama kwa zaidi ya saa moja wakti wanaume ndani ya nusu saa walikuwa washapata mshindi.
Meneja Mkuu wa Radio Efm na Tv E, Dennis Busulwa(Sebo), akizungumza kabla ya kukabidhi kadi kwa washindi wa Pikipiki wa shindano la Shika Ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam
Mshindi wa Shindano la Shika Ndinga kwa Wanawake kwa mkoa wa Dar es Salaam Ashura Ramadhani mkazi wa Bunju Akiwa jjuu ya pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa na Efm. 
Mshindi wa Shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa Wanaume Abbas Awadhi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala akiwa juu ya Pikipiki yake mara baada ya kutangazwa mshindi
wanawake waliongia fainali katika shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam wakichuana wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
Wanaume waliongia fainali katika shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam wakichuana wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
washiriki wa shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam wakichuana wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
Msanii wa Muziki wa Singeli nchini Man Fongo, akitumbuiza katika shindano la shika ndinga kwa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa shindano hilo lililofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga
Wakazi wa Dar es Salaam waliofika kushuhudia shika ndinga katika Viwanja vya Mwembeyanga


Hivyo makala WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM

yaani makala yote WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/wawili-waondoka-na-bodaboda-shika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAWILI WAONDOKA NA BODABODA SHIKA NDINGA DAR ES SALAAM"

Post a Comment

Loading...