Loading...

WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI

Loading...
WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI
link : WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI

soma pia


WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI

*Ni baada ya kubainika kwa tofauti ya zaidi ya Shilingi bilioni 30 ambayo ni pungufu ya fedha ambayo Serikali imekiri kupokea.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Madini Angella Kairuki amezindua rasmi Ripoti ya Nane ya Taasisi ya Uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini mafuta na gesi asilia nchini Tanzania(TEITI) kwa mwaka 2015/2016 ambayo inazungumzia ulinganishi wa mapato  ya Serikali na malipo ya kampuni za madini, mafuta na gesi asilia huku akitoa maagizo  kwa taasisi hiyo kuhakikisha ripoti hiyo inapelekwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) baada ya kubainika kuna tofauti ya  zaidi ya Shilingi bilioni 30.
Amefafanua Ripoti ya TEITI inaonesha kuwa kuanzia Julai 1 mwaka 2015 hadi Juni mwaka 2016 kunaonesha jumla ya Sh.434,627,874,380 zimepokelewa serikalini kutoka kampuni 55 za madini , mafuta na gesi asilia zilizoshiriki kwenye mchakato huo wa ulinganishi ambapo kampuni hizo zinaonesha zililipa  serikalini Sh 465,164,747,725 na hivyo kusababisha tofauti kati ya malipo kuwa ni pungufu Sh 30,536,873,345 chini ya fedha ambazo Serikali inakiri kupokea.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Waziri Kairuki amepongeza kazi nzuri ya TEITI ya kukamilisha ripoti hiyo lakini ni lazima ifahamike imekuaje imejitokeza tofauti hiyo ya fedha na hivyo ametoa maelekezo taarifa hiyo ipelekwe kwa CAG kwa ajili ya uchunguzi kama kifungu 18(1) cha sheria ya TEITI ya mwaka 2015 kinavyotoka.
"Tunataka hii ripoti iende kwa CAG ili tujue nini ambacho kimetokea na ni vema kazi hiyo ikafanyika kwa wakati,"amesema Waziri Kairuki.
Pia amesema ripoti hiyo  inaonesha sekta ya madini imechangia kwa asilimia 85 na sekta ya mafuta na gesi asilia ikionesha kuchangia asilimia 15 ya mapato ya Serikali kwa mwaka 2015,2016.
Amefafanua kuwa yote ambayo yamependekezwa na kamati ya TEITI yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha yale ambayo yamesemwa yanafanyika kama ambavyo wamependekeza kwa maslahi ya Watanzania wote huku akielezea hatua kadhaa ambazo Serikali inachukua kuhakikisha madini yananufaisha wananchi wote.
Waziri Kairuki ameeleza nchi yetu ilijiunga katika mpango wa kimataifa wa Uwazi katika sekta ya uchimbaji wa rasilimali ambapo lengo lake kuu lilikuwa kuhakikisha mapato yanayopatikana katika sekta hiyo yanajulikana wazi kwa wananchi bila kificho.Hivyo  Serikali na kampuni za madini yanawajibika kutoa taarifa zake kwa umma ili ufahamu kilichopatikana na hatimaye wataweza kuhoji ni kwa namna gani wanafanufaika na rasilimali hizo.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya nane ya TEITI  ya ulinganishi wa Mapato ya Serikali na Malipo ya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi asilia kwa mwaka wa fedha 2015/16 leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi wa Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini Mafuta na Gesi Asilia nchini Tanzania(TEITI), Augustina Rutahiwa akizungumzia mchakato ulivyofanyika ili kupata ripoti iliyonzuri wakati wa uzinduzi wa ripoti ya nane ya TEITI  ya ulinganishi wa Mapato ya Serikali na Malipoya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi asilia kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akizungumzia serikali ivyojipanga kulinda madini ya hapa nchini kuwanufaisha hasa wazawa wakati wa mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya nane ya TEITI uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Msimamizi wa kujitegemea, Symphorian Malingumu akiwasilisha ripoti ya nane ya TEITI  ya ulinganishi wa Mapato ya Serikali na Malipo ya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi asilia kwa mwaka wa fedha 2015/16 leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya nane ya TEITI  ya ulinganishi wa Mapato ya Serikali na Malipo ya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi asilia kwa mwaka wa fedha 2015/16 leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka Makampuni, Asasi za Kiraia na Taasisi za Serikali wakiwa wameshika ripoti ya nane ya TEITI  ya ulinganishi wa Mapato ya Serikali na Malipo ya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi asilia kwa mwaka wa fedha 2015/16  mara baada ya kuzinduliwa leo.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe kutoka Makampuni, Asasi za Kiraia na Taasisi za Serikali walioshiriki katika mchakato wa ripoti  ya nane ya TEITI  ya ulinganishi wa Mapato ya Serikali na Malipoya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi asilia kwa mwaka wa fedha 2015/16 leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI

yaani makala yote WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/waziri-wa-madini-aagiza-ripoti-ya-teiti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI WA MADINI AAGIZA RIPOTI YA TEITI IPELEKWE KWA CAG KWA AJILI YA UCHUNGUZI"

Post a Comment

Loading...