Loading...
title : WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA
link : WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA
WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agnes Kijo amesema ipo haja kwa wazalishaji wa dawa kuhakikisha wanazalisha dawa zenye ubora kwa kuzingatia viwango vilivyoanishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Kijo ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watalaam wa dawa katika viwanda yaliyofanyika makao makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam , ambapo amefafanua nia ya mafunzo yanayotolewa ni kwa ajili ya kuzalisha dawa bora, vifaa tiba na vitendanishi.
Amesema kuelekea uchumi wa viwanda ni pamoja na viwanda vitakavyojengwa ni lazima kufuata matakwa yaliyoanishwa na mamlaka za kudhibiti ubora huo ikiwemo TFDA.
Amesema uwezo wanawajengea ni kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo ni dawa, vifaa tiba pamoja na vitanishi kutokana na uzoefu wa WHO katika masuala ya ukaguzi wa viwanda .
Aidha amesema mafunzo hayo yakifanyiwa kazi itakuwa ni rahisi katika kufikia ubora ambao ndio unatakiwa kwa WHO katika kulinda afya ya mlaji.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na dawa(TFDA), Agnes Kijo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuwajengea uwezo watalaam wa dawa katika viwanda na watendaji wa mamlaka hiyo yaliyofanyika Makao Makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa Mshauri katika Uimarishaji wa wa Mamlaka za Udhibiti wa Dawa wa Shrika la Afya Duniani, Mohamed Refaat akizungumza kuhusiana na mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa dawa katika viwanda ili kuweza kuzalisha dawa zenye ubora , mafunzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa Mshauri katika Uimarishaji wa wa Mamlaka za Udhibiti wa Dawa wa Shrika la Afya Duniani, Mohamed Refaat akitoa maelezo kwa watendaji wa TFDA na wataalam wa dawa katika viwanda katika mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Makao Makuu ya TFDA jijiji Dar es Salaam.
Sehemu ya watendaji na wataalam wa dawa katika viwanda wakiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo na Shirika la WHO yaliiyofanyika Makao Makuu ya TFDA jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA
yaani makala yote WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/who-yawajengea-uwezo-watendaji-wa-tfda.html
0 Response to "WHO YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WA TFDA NA WATALAAM WA DAWA KATIKA VIWANDA"
Post a Comment