Loading...
title : Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China
link : Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China
Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China
Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Ujenzi ya Nchini China ya Civil Engineering Construction Corporation 'CCECC' Bw. Zhuang Shangbiao alisema hatua iliyochukua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar 'SMZ' ya kuipa kazi ya ujenzi wa barabara Nchini imeleta heshima kubwa na ya kipekee kwa Kampuni hiyo.
Alisema kazi iliyo mbele kwa uongozi na wahandisi wa kampuni hiyo hivi sasa ni kujipanga vyema katika kuhakikisha heshima waliyopewa na SMZ wanailinda katika kuwajibika ipasavyo wakati wa utekelezaji wa jukumu hilo zito katika misingi ya ari na bidii kubwa.
Bwana Zhuang Shangbiao akiuongoza Ujumbe wa Viongozi saba wa Taasisi hiyo ya Civil Engineering Construction Corporation alisema hayo wakati akitoa shukrani katika mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema uzowefu wa ujenzi iliyokuwa nayo Kampuni hiyo ya CCECC kwa zaidi ya Miaka 50 iliyopita inahamishiwa Zanzibar katika ujenzi wa barabara inayoanzia Bububu, Mahonda kupitia Kinyasini hadi Mkokotoni yenye urefu wa Kilomita 31.
Bwana Zhuang alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wahandisi wa Ujenzi wa Kampuni ya CCECC watakamilisha kazi hiyo kwa wakati ulliopangwa na katika kiwango kinachokubalika Kimataifa kwa vile wana utaalamu na uzoefu wa kutosha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya Civil Engineering Construction Corporation 'CCECC' ya China Bw. Zuang Shangbiao Vuga Mjini Zanzibar.
Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China Bw. Zuang Shangbiao wa tatu kutoka Kulia akielezea shukrani zake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuiamini Kampuni yake kujenga Bara bara ya Bububu hadi Mkokotoni kupitia Mahonda na Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud Mohamed.
Balozi Seif kushoto akisifu umahiri wa Kampuni za Kichina zinazofanya kazi Nchini Tanzania wakati akibadilishana mawazo na Rais wa Kampuni ya CCECC Bw. Zhuang Shangbiao aliyekaa upande wa Kushoto.
Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China Bw. Zuang Shangbiao Kushoto akimkabidhi zawadi ya picha ya Ukuta Mkuu wa China 'Great Wall' Balozi Seif mara baada ya mazungumzo yao.
Bwana Zuang Shangbiao Kushoto akifurahia zawadi ya viungo aliyokabidhiwa na Balozi Seif baada ya mazungumzo yao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China
yaani makala yote Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/balozi-seif-akutana-na-kufanya_18.html
0 Response to "Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China"
Post a Comment