Loading...
title : BARA ZA LA MADIWANI UBUNGO LAPOKEA TAARIFA ZA KAMATI NA MAPENDEKEZO
link : BARA ZA LA MADIWANI UBUNGO LAPOKEA TAARIFA ZA KAMATI NA MAPENDEKEZO
BARA ZA LA MADIWANI UBUNGO LAPOKEA TAARIFA ZA KAMATI NA MAPENDEKEZO
Mwambawahabari
Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa robo ya tatu ya mwaka (Januari – Machi 2018) umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Kibamba, ambapo kamati mbalimbali zimewasilisha taarifa zake.
Katika Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti ambaye ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, jumla ya kamati tano zimeweza kuwasilisha taarifa zake. Kamati hizo ni pamoja na: Kamati ya Afya, Kamati ya Fedha na Uongozi, Kamati ya Maadili, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira, na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi.
Kwa upande wa kamati ya Fedha na Uongozi, imewasilisha taarifa yake na kutoa maazimio ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi. Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na kumtaka Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi kuwasilisha orodha ya miradi ya maendeleo iliyo katika taratibu za manunuzi, taarifa za mapato na matumizi za robo ya pili na tatu zifanyiwe marekebisho ili zisitofautiane na mwenendo wa taarifa za robo ya kwanza.
Kwa upande wa kamati ya maadili imewasilisha taarifa yake na kusema hakuna malalamiko ya kimaadili iliyopokea kwa njia ya maandishi.
kamati ya mipango miji na mazingira imetoa mapendekezo ikiwemo kufuatilia migogoro ya ardhi, Huku Kamati ya Afya ikifuatilia ujenzi wa Zahanati mbalimbali.
Kwa upande wake Kamati ya Kudhibiti Ukimwi imetoa mapendekezo kwa viongozi wa dini kukutana na kamati hiyo ili kuweza kujadiliana namna ya kuwasaidia wagonjwa ambao wamekuwa wakisitisha matumizi ya dawa za ARV kwa sababu yakufanyiwa maombi.
Hivyo makala BARA ZA LA MADIWANI UBUNGO LAPOKEA TAARIFA ZA KAMATI NA MAPENDEKEZO
yaani makala yote BARA ZA LA MADIWANI UBUNGO LAPOKEA TAARIFA ZA KAMATI NA MAPENDEKEZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARA ZA LA MADIWANI UBUNGO LAPOKEA TAARIFA ZA KAMATI NA MAPENDEKEZO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/bara-za-la-madiwani-ubungo-lapokea.html
0 Response to "BARA ZA LA MADIWANI UBUNGO LAPOKEA TAARIFA ZA KAMATI NA MAPENDEKEZO"
Post a Comment