Loading...

BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000

Loading...
BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000
link : BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000

soma pia


BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000

*Maombi yote kupokelewa kwa njia ya mtandao, kurugenzi ataja vipaumbele 
*Wenye ulemavu, yatima kupewa kipaumbele, RITA nao kuhakiki cheti cha kuzaliwa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) imesema mwaka wa masomo wa 2018/2019 wamejipanga kutoa mikopo kwa jumla ya wanafunzi wapya 40,000 na wanaoendelea zaidi ya 80,000 huku ikitangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa muda wa miezi miwili na maombi yote yatapokelewa kwa njia ya mtandao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Abdul -Razaq Badru wakati anatangaza kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa miezi miwili na kufafanua jumla ya Sh.bilioni 427 zimetengwa.

Kuhusu maombi ya mkopo, Badru amesema leo wametangaza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu na maombi yote yawe kwa njia ya mtandao.

Amesema maombi hayo yatatumwa kupitia www.olas.heslb.go.tz na ni kuanzia leo hadi Julai 15 mwaka huu ili kuwapa fursa wanafunzi wahitaji kuwasilisha maombi hayo.

"Mwaka jana tulitoa mwezi mmoja,mwaka huu tumetoa muda wa zaidi ili kuwawezesha kusoma mwongozo kwa makini na kuzingatia maelekezo tunayopewa,"amesema Badru.

Amefafanua kuwa mwongozo huo kuna mambo muhimu yakiwamo ya sifa na taratibu za utoaji mikopo kwa mwaka 2018/2019.Mwongozo huo unapatikana katika lugha ya Kiswahili na Kingereza kwenye tovuti ya www.heslb.go.tz.

Amesema mambo muhimu yaliyomo kwenye mwongozo  ni kwamba kipaumbele kitatolewa kwa Watanzania wahitaji wanaosoma kozi zenye uhitaji mkubwa zaidi  kitaifa kama walimu wa masomo ya sayansi na hisabati, na sayansi ya afya ya binadamu.

Amesisitiza watatoa kipaumbele pia kwa wahitaji ambao ni yatima na wana nakala za vyeti vya vifo vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili na Udhamini (RITA) nao watapewa kipaumbele bila kujali kozi wanazosoma. Pia wengine watakaopewa kipaumbele ni waombaji wenye ulemavu uliothibitishwa na Mganga wa Mkoa au wilaya.
Mkurugenzi Mtendahi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul -Razaq Badru (kulia) akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuhusu kutangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 leo Alhamisi, Mei 10, 2018 jijini Dar es salaam. Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na kushoto Meneja Usajili wa RITA, Patricia Mpuya. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000

yaani makala yote BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/bodi-ya-mikopo-elimu-ya-juu-kutoa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000"

Post a Comment

Loading...