Loading...
title : Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni
link : Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni
Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni
Serikali imeona umuhimu wa kuingiza elimu ya mlipa kodi kwenye mitaala ya elimu nchini ili kwajengea Watanzania tabia, mwenendo na mazoea ya kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Lupembe Mhe. Joram Ismael Hongoli juu ya kwa nini Serikali isiingize kwenye mitaala ya elimu somo la umuhimu wa kulipa kodi ili lifundishwe kuanzia shule ya msingi ili wananchi wapate uelewa wa kodi na waweze kulipa kodi kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.
"Serikali inatambua umuhimu wa elimu ya mlipa kodi katika kumjengea mwananchi tabia ya kulipa kodi. Katika somo la Uraia na Maadili kuanzia darasa la III na kuendelea, mtaala umelenga kumjengea na kumuandaa mwanafunzi kuwa mwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya kila siku," alisema Mhe. Ole Nasha.
Vile vile mtaala umelenga kumjengea mwanafunzi kuiheshimu na kuithamini jamii yake kwa kuwa mwadilifu na mzalendo ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu ya kitaifa ikiwemo kulipa kodi.
Aidha amesema, kutokana na umuhimu wa kuwajengea vijana utamaduni wa kulipa kodi, elimu ya mlipa kodi ni jambo muhimu, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikisha Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) itaendelea kuboresha elimu hiyo ili isisitizwe na kuwekewa mkazo katika mitaala ya elimu kuanzia elimu ya Msingi.
Hivyo makala Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni
yaani makala yote Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/elimu-ya-mlipa-kodi-kutolewa-mashuleni.html
0 Response to "Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni"
Post a Comment