Loading...
title : Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu
link : Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu
Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imekabidhi jengo la maabara kwa Shule ya Sekondari Mangu iliyopo Kata ya Shagihilu baada ya ujenzi wake kukamilika.
Maabara hiyo iliyokamilika gharama ya thamani ya Sh. Milioni 10.1 linatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo wa mchepuo wa sayansi kwa vitendo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akikabidhi jengo hilo alisema litachochea ufaulu wa wanafunzi ambao awali walikosa mazoezi ya vitendo.
Alisema lengo la Halmashauri ni kuhakikisha elimu inakua na hivyo inaendelea kuboresha miundombinu ya shule zake ikiwemo ujenzi wa maabara kwa ajili ya sayansi.
Mang’era Mang’era aliwataka walimu na wanafunzi kuwa kitu kimoja na kuitendea haki maabara hiyo kwa kushirikiana ili wawe na ufaulu mzuri katika mitihani inayohusisha mazoezi ya vitendo.
Alisema kuwa ufaulu kwa wanafunzi katika shule hiyo na zingine utafaleta sifa kwa wananchi wa kata hiyo pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa ujumla.
Mang’era ambaye pia ni Afisa Mipango aliwataka wanafunzi kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yao ya baadaye katika kitaaluma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la maabara Shule ya Sekondari Mangu.
Viongozi mbalimbali wakiangalia maabara ya Shule ya Sekondari Mangu baada ya kuziduliwa rasmi na kukabidhiwa baada ya ujenzi wake kukamilika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era (kulia) akiwa na Afisa Elimu Sekondari, Paul Kasanda wakiangalia vifaa mbaimbali vya maabara hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mangu (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya jengo la maabara.
Diwani wa Kata ya Shagihilu, Mhe. Mohamedi Amani akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo.
Muonekano wa maabara hiyo wakati viongozi mbalimbali walipotembelea baada ya kufunguliwa rasmi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu
yaani makala yote Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/halmashauri-ya-kishapu-yakabidhi.html
0 Response to "Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu"
Post a Comment