Loading...

KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI

Loading...
KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI
link : KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI

soma pia


KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI

*Rais wa kampuni hiyo atua nchini, afanya mazungumzo ya kina na TIC

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC)kimefanya mazungumzo ya kina na Kampuni ya Goan Cable Co.LTD ambayo inataka kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme kwa kujenga kiwanda cha kutengeneza nyaya nchini.

Mazungumzo kati ya TIC yamefanyika Mei 2 mwaka huu jijini Dar es Salaam baada ujumbe wa watu wanne wanaokiongozwa na Rais wa Kampuni Jael In Yoon kufika nchini na kujadiliana na kituo hicho katika masuala ya uwekezaji katika eneo hilo. 

Taarifa ya TIC kwa vyombo vya habari ambayo imetolewa leo jijini Dar es Salaam imesema Kampuni ya Gaon Cable Co. Ltd ni kongwe na imebobea katika utengenezaji wa nyaya za umeme mkubwa na wa kati huko Korea ya Kusini. 

Na kwamba kampuni hiyo pia imehusika katika kutengeneza miundombinu ya kusambaza umeme Korea ya Kusini kwa zaidi ya miaka 60.TIC imefafanua ujio wa wafanyabiashara hao umefanyika kutokana na kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Korea Kusini lililoandaliwa na kituo hicho kwa kushirikiana na na Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

"Kongamano hilo la kibaishara kati ya Tanzania na Korea Kusini lilifanyika Januari 31 mwaka huu katika mji wa Seoul,"imeeleza.Imefafanuliwa lengo la ziara ya ujumbe wa kampuni hiyo ni kuangalia fursa za uwekezaji katika maendeleo ya sekta ya nishati hasa kufungua kiwanda cha kutengeneza nyaya nchini.

Pia ujumbe huo umekuja nchini ili kuonana na taasisi husika katika sekta ya nishati ili kufanya mazungumzo na kupata miongozo ya kuanzisha kiwanda hicho."TIC imefanya mkutano na wafanyabiashara hao na kuwapa taarifa zote muhimu.Pia kuwahakikishia utayari wa kuwasidia katika hatua zote za uanzishaji mradi huo.

"Ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja. Huduma hizo ni pamoja na usaidizi wa kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji, kuandikisha Kampuni, kujisajili na VAT, TIN, Kupata Leseni ya biashara na vivutio vya uwekezaji.

"Pia kibali cha kazi daraja A na C, hati za ukazi daraja A na B, kusajiliwa kwa ajili ya kupata viwango vya ubora (TBS),cheti cha uwezekaji, kutathmini masuala yahusuyo mazingira (NEMC), kusaidiwa kupata vibali vya usalama mahala pa kazi (OSHA) na Kusaidiwa upatikanaji wa vibali kwa uwekezaji unaohusisha chakula na dawa (TFDA),"imesema TIC katika taarifa yake.

Wakiwa nchini, wageni hao pia walifanya mikutano na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka yaUkanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa majadiliano na miongozo zaidi ya kuwekeza katika sekta ya umeme pamoja na kupata eneo la kuweka mradi huo. 

TIC imesisitiza uanzishwaji wa kiwanda hicho nchini utakuwa na mchango mkubwa si tu katika kukuza uchumi, kutengeneza ajira, kupunguza uagizaji wa nyaya bali pia kuimarisha njia za usambazaji wa umeme nchini pamoja na nchi jirani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe (kushoto) akiwa  na Rais wa Kampuni ya Gaon Cable Jael Yoon baada ya kufanya mazungumzo kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI

yaani makala yote KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/kampuni-ya-goan-cable-coltd-ya-korea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI"

Post a Comment

Loading...