Loading...
title : KESI INAYOMKABIRI WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU YAKWAMA
link : KESI INAYOMKABIRI WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU YAKWAMA
KESI INAYOMKABIRI WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU YAKWAMA
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuanza kusikiliza utetezi wa msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya, sababu amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.
Taarifa hiyo imewasilishwa mahakamani hapo na Mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali, Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani.
Wakili Kakula alidai, kesi hiyo leo Mei 29/2018 ilikuja kwa ajili ya mshtakiwa Wema kuanza kujitetea lakini anashangaa kutokumuona mahakamani hapo kwani hata ahirisho la mwisho la kesi yake hakuwepo.
Kufuatia hayo, Mama Wema alisimama na kutoa nyaraka za Wema za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.Wakili Kakula alidai kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba mahakama isimamie sheria.
Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema ni kweli hakuna uthibitisho, hivyo katika tarehe ijayo uthibitisho unapaswa kuwepo, na kesi imeahirishwa hadi June 13/ 2018.Mbali na Wema, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni wafanyakazi wa Wema, Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya.Inadaiwa Februari 4, 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February mosi 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.
Hivyo makala KESI INAYOMKABIRI WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU YAKWAMA
yaani makala yote KESI INAYOMKABIRI WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU YAKWAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI INAYOMKABIRI WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU YAKWAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/kesi-inayomkabiri-wema-sepetu-mahakama.html
0 Response to "KESI INAYOMKABIRI WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU YAKWAMA"
Post a Comment