Loading...
title : MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA
link : MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA
MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MBUNGE wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)Mchungaji Peter Msigwa ameamua kutema nyongo na kuweka wazi namna ambavyo anafurahishwa na utendaji kazi wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli.
Mchungaji Msigwa amevunja ukimya na kuamua kumsifu Rais jana akiwa mkoani Iringa ambapo alipata nafasi ya kualikwa kwenye chakula kilichoandaliwa na Rais kwa wazee wa Mkoa huo ambapo mbunge huyo alikuwa miongoni mwa walioalikwa na waliopata nafasi ya kuzungumza mbele ya Rais.
Akizungumza jana mkoani Iringa Mchungaji Msigwa amesema Rais Dk.Magufuli amekuwa akisisitiza kwenye hotuba zake kuwa yeye hajali mambo ya vyama na hilo limedhihirika kuwa ni kweli hajali vyama.
"Umesaidia sana , fedha za kutoka kwako zimekuja nyingi, kama alivyosema Waziri Mahiga, kuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais, umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu Sh.bilioni 3.5.
"Tuna stendi nzuri ipo Ipogoro ya karibu Sh.bilioni 3, tuna maji, kwa hiyo kuna vitu vimefanyika kwa kweli mheshimiwa Rais hupendelei.Fedha zinakuja hata sisi ambao ni wa Chadema unaleta fedha, kwa hiyo tunakupongeza sana kutokana na juhudi zako za kuleta maendeleo ,"amesema Mchungaji Msigwa.
Wakati anazungumza hayo kulikuwa kimya huku baadhi ya wageni waalikwa kwenye chakula hicho wakifurahia kwa chini chini.Hata hivyo baadhi ya wadau wa siasa nchini wamesema kilichofanywa na mbunge huyo ni katika kuthibitisha kutoka kwenye moyo wake kuwa kuna mambo mengi mazuri ambayo Rais anafanya bila upendeleo.
Hata hivyo ni wazi Mchungaji Msigwa sasa anaingia kwenye orodha ya wabunge ambao wamefurashwa na utendaji kazi wa Rais .Historia ya Mchungaji inaonesha hajawahi kusifu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano lakini hatimaye amekubali kuwa kazi inafanyika kwa maendeleo ya Watanzania wote.

Hivyo makala MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA
yaani makala yote MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/mchungaji-msigwa-avunja-mwiko-amsifu.html
0 Response to "MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA"
Post a Comment