Loading...
title : Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini
link : Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini
Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini
Wapenzi wa Soka vijiji kufurahia michuano ya Kombe la dunia mwaka huu. Hii ni kutokana na Kampuni ya Star Times ambayo ina mkataba hapa nchini wa kutangaza mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2018, yatakayofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi ujao, Kampuni hiyo imeingia ushirikiano na kampuni ya kusambaza nishati ya jua na vifaa vinavyotumia nishati hiyo ya Mobisol, kutumia mtandao wake kuwezesha wananchi wanaoishi maeneo yasio na umeme wanaotumia nishati ya umeme wa jua nchini na nchi jirani za Kenya na Uganda kutokupitwa na mashindano hayo ya kihistoria duniani kote.
Ushirikiano huo ambao umetangazwa jijini Dar es Salaam leo unawezesha wateja wanaotumia umeme na vifaa vya Mobisol kununua vifaa maalumu vya kuboresha mawasiliano vitakavyowezesha kushuhudia mechi za kombe la dunia, sambamba na kupata chaneli mbalimbali za burudani kupitia vingamuzi vya Star Times.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mobisol Tanzania,Patric Juma,ameeleza kuwa wateja wa Mobisol nchini, wanaweza kununua vifaa vya mawasiliano kutoka star Times vitakavyowawezesha kufurahia burudani hiyo ya soka bure na kwa wakati wote kuanzia sasa hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu.Vifaa hivyo baada ya kununuliwa wanafungiwa bure popote walipo.
“Tunafurahia kuingia ushirikiano huu na Star Time,hasa kwa kuwaletea ofa maalumu wananchi wanaotumia umeme wa nishati ya jua maeneo mengi yasiyo na umeme ili kuwawezesha kupata burudani za mashindano ya Kombe la Dunia ,Mobisol tutahakikisha tunaendelea kusambaza umeme kwenye maeneo yasio na nishati hiyo sambamba na kubuni vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati ya jua”Alisema Patric Juma.
Makamo wa Rais wa Startimes,Zuhura Hanif(kulia)akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu (wapili kushoto)baada ya Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Wengine kushoto ni Meneja wa Mobisol Lynda Okoko pamoja na Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa.Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kampuni ya Umeme wa Jua-Mobisol,Lynda Okoko(kushoto)akipeana mkono na Makamo wa Rais wa Startimes kuashiria Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi,Wengine katika picha wapili kushoto ni Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa na Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kampuni ya Umeme wa Jua-Mobisol,Lynda Okoko, Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa,Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu pamoja na Makamo wa Rais wa Startimes Zuhura Hanif,wakionyesha vipeperushi vyenye chaneli mbalimbali zitakazorusha kombe la Dunia wakati wa Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu(kushoto)akiwaonesha vifaa vya umeme wa Jua,Makamu wa Rais wa Startimes Zuhura Hanif na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa,vitakavyotumika kurusha soka msimu wa Kombe la Dunia 2018 wakati wa Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo hiyo msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini
yaani makala yote Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/mobisol-na-startimes-kuleta-shangwe-za.html
0 Response to "Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini"
Post a Comment