Loading...
title : RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI
link : RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI
RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chai Tanzania (Tea Board of Tanzania – TBT).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote umeanza tarehe 21 Mei, 2018.
Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Research Institute – TARI).
Uteuzi wa Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo umeanza tarehe 22 Mei, 2018 na kabla ya uteuzi huu, alikuwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Mashariki, Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ilonga Mkoani Morogoro.
Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fidelis Angelo Myaka ambaye amestaafu.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Mei, 2018
Hivyo makala RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI
yaani makala yote RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/rais-dkt-magufuli-afanya-uteuzi-wa.html
0 Response to "RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI"
Post a Comment