Loading...

RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka

Loading...
RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka
link : RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka

soma pia


RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetaja idadi  ya watalii walioingia nchini kuwa imeongezeka kutoka Milioni 1.2 Mwaka 2016 hadi kufikia watalii Milioni 1.3 mwaka 2017 huku watalii kutoka nchini Marekani wakiwa vinara.Hatua hiyo inakuja ikiwa ni  kukua kwa kasi ya uchumi huku  ikisaidiwa na ujenzi wa miundombinu ya barabara katika hifadhi za  Taifa.
Mbali na  idadi hiyo, Serikali imetaja  mapato  yaliyopatikana kutokana na watalii hao kuwa yameongezeka kutoka wastani wa Dola za Kimarekani Milioni 2.1 Mwaka 2016 hadi kufikia Dola Milioni 2.2 Mwaka 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudance Milanzi amesema taarifa ya utafiti huo unaonesha kuwa Tanzania inazidi kufanya vizuri katika sekta ya utalii kwa vile kila mwaka idadi ya watalii na mapato yamekuwa yakiongezeka.
Awali, Milanzi  alisema ripoti hiyo ya pamoja iliandaliwa   kwa ushirikiano wa Benki Kuu Tanzania(BOT), Tume ya Taifa ya Takwimu(NBS), Idara ya Uhamiaji Zanzibar,
Kwa mujibu wa Milanzi, ripoti hiyo iliyopatikana kutokana na ‘survey’ iliyofanywa  katika njia kuu za watalii, ikiwemo viwanja vya ndege pamoja na maeneo ya njia za mipaka ya kuingia nchini, pia imebaini idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini wanatoka katika nchi za Marekani, Uingereza, India, Uholanzi pamoja na Uswiswi.
Katika uzinduzi wa taarifa hiyo Milanzi amesema taarifa hizo zilikusanywa  kupitia  viwanja vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro(KIA), Abeid Aman Karume(Zanzibar) pamoja na mipaka ya Namanga, Tunduma, Mtukula na kwingineko, kwa kiasi kikubwa imechangiwa na idadi ya  watalii walioingia nchini na kutembelea fukwe pamoja wanyamapori
Alisema kimsingi ongezeko la watalii waliongia nchini, pia limetokana na kasi ya kuvitangaza vivutio mbalimbali vilivyopo nchini inayofanywa  na Bodi ya Utalii Tanzania(TTB)  kupitia mamlaka iliyopewa ya kuvitangaza vivutio hivyo, zikiwemo mbuga za wanyama, fukwe, mlima Kilimanjaro na vinginevyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu za watalii nchini kwa mwaka 2017 inayoonesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa mwaka 2017.  Kulia ni Kamishina wa Idara ya Uhamiaji, Hannelore Manyanga na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) Dkt. Albina Chuwa

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsius Mdamu akizungumza kuhusiana na kukua kwa kasi kwa utalii wa fukwe na jinsi Idara ilivyojipanga kuimarisha fukwe zilizopo nchini wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu za watalii nchini kwa mwaka 2017, inayoonesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa 2017.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Paskas Mwiru (katika) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya kutathimini twakimu za watalii wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu ya watalii waliokuja nchini kwa mwaka 2017, uliofanyika leo jijini Dar es Salam
wadau wa sekta ya  Utalii wakiwa kwenye kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam cha uzinduzi wa taarifa ya takwimu  ya watalii waliokuja nchini kwa mwaka 2017 huku ikionesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa 2017.
Picha na habari na Lusungu Helela- MNRT



Hivyo makala RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka

yaani makala yote RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/ripoti-idadi-ya-watalii-walioingia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RIPOTI: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Yaongezeka"

Post a Comment

Loading...