Na George Binagi
Mwambawahabari
Timu ya soka ya wasichana wanaoishi katika mazingira magumu TSC Sport Academy (Tanzania Street Children) ya Jijini Mwanza imepokelewa kwa kishindo hii leo katika uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kutwaa nafasi ya pili ya michuano ya kombe la dunia 2018 ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Urusi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella ameongoza mapokezi hayo ambapo amesema hatua hiyo inapaswa kuleta changamoto kwa timu nyingine kufanya vizuri katika michuano mbalimbali huku akiwahimiza wadau wa michezo kushirikiana na serikali kuendeleza michezo mkoani Mwanza.
“Tumefurahi kwa ushindi tulioupata maana tuliahidi tunaenda kupambana na ndicho kitu tulichokifanya kwa hiyo tunafurahi kuja na ushindi”. Amesema nahodha wa timu ya TSC huku akifurahia mapokezi waliyopewa.
Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL na mlezi wa timu hiyo, Altaf Mansoor ameipongeza kwa ushindi huo na kubainisha kwamba TSC imekuwa kitovu cha kuibua na kuendeleza wachezaji wengi na baadhi yao wanachezea timu mbalimbali ikiwemo Simba huku wengine wakipata fursa ya za kimasomo.
Michuano hiyo imemalizika nchini Urusi ambapo timu ya wasichana TSN imeshika nafasi ya pili baada ya kufungwa kwa tabu goli 1-0 na wenzao kutoka nchini Brazir.
Itakumbukwa mwaka 2010 nchini Afrika Kusini timu wavulana TSC ilishika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo, mwaka 2014 ikabeba kombe nchini Brazil.
Mkuu wa mkoa Mwanza John Mongella (mwenye kombe) pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya wasichana TSC Sports Academy.
Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL na mlezi wa timu hiyo, Altaf Mansoor (mwenye kombe) akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL na mlezi wa timu hiyo, Altaf Mansoor, wanafamilia pamoja na wadau wa michezo wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu hiyo.
Ahmed Misanga ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi ya First Community na mwakilishi wa mbunge Jimbo la Nyamagana akiwa na kombe.
Mwanahabari wa Dira Media, Charles Mseti akiwa na kombe.
Mwanahabari wa ITV, Mabere Makubi naye alikuwepo.
Viongozi na wadau wa michezo mkoani Mwanza.
Kombe limerejea nyumbani.
Wadau wa michezo Jijini Mwanza na kombe.
Tunafurahia kombe letu.
Wadau wa michezo mkoani Mwanza.
Timu hii pia ilipokelewa na viongozi na wadau wa michezo katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL na mlezi wa timu hiyo, Altaf Mansoor na wadau wengine wakifurahia kombe kurejea nyumbani.
Viongozi wa michezo mkoani Mwanza, wadau mbalimbali pamoja na wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja.
0 Response to "TIMU YA MPIRA YA WASICHANA ILIYO WAKILISHA TANZANIA KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI YAPOKELEWA KISHUJAA MWANZA."
Post a Comment