Loading...
title : TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'.
link : TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'.
TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mbio za Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo, Mbio hizo Zimeshirikisha wanariadha mbalimbali wakiwemo wakenya na watanzania pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi wa mkoa wa Mbeya , kumekuwepo na washiriki wa mbio mbalimbali zikiwemo za Kilomita 41, kilomita 21, Kilomita 5, Kilomita 2, Mita 100, Mita 400 na Mita 800.
Dk. Tulia Akson Naibu Spika wa Bunge amewashukuru wadhamini mbalimbali ambao wamewezesha kufanyika kwa mbio hizo kwa mafanikio makubwa mbali ya changamoto ndogondogo ambazo zitaendelea kuboreshwa katika maandalizi ya mbio zingine zitakazofanyika mwakani jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akianzisha Mbio za mita 100 katika mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizowahusisha viongozi wa serikali , Wabunge na Madiwani kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo,
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku pamoja na baadhi ya wabunge wakishiriki mbio za mita 100 kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati wa mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 jijini Mbeya.
Watoto wakishiriki mbio za mita 1500.
Washiriki wa mbio za Baiskeli Kilomita 150 wakiingia uwanja wa Sokoine mara baada ya kumaliza mbio hizo.
Hivyo makala TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'.
yaani makala yote TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/tulia-awashukuru-wadhamini-kwa.html
0 Response to "TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KWA KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'."
Post a Comment