Loading...
title : UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA
link : UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA
UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA
Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
SERIKALI kupitia Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Joseph Kakunda ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam kwa kuwa Halmshauri ya kwanza na ya mfano kwa kutoa fedha za mikopo ya wanawake na vijana kwa asilimia 100, kutoka katika
mapato ya ndani.
Hivyo Naibu Waziri ameitaka Wizara ya TAMISEMI kuandikia Manispaa ya Ubungo barua ya pongezi,kwani maeneo mengine ni jambo ambalo linaonekana kugumu kutekelezeka lakini Ubungo
wameweza.
Manispaa ya Ubungo juzi wamezindua mchakato wa ugawaji wa mikopo ya Sh.bilioni 1.94 ,wakati ina mwaka Mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.Akizungumza fedha hizo Meya Ubungo Boniface Jacob
,amesisitiza mikopo itatolewa kwa vigezo bila kuangalia dini,kabila wala chama cha mtu.
"Waosema mikopo ni Ilani ya CCM,wajiulize mbona kwingine kuna Halmashauri za CCM lakini hakuna mambo haya mazuri? Hivyo watu wajue kuna viongozi makini na imara wanatoka chama cha Chama cha Upinzani upinzani na ndio msingi na chachu ya mafanikio,"amesema Jacob.
Jacob ametoa rai kwa vijana kuomba mikopo hiyo,kwani idadi ya akina mama ni kubwa kuliko idadi ya vijana,huku akiahidi Mei mwaka huu halmashauri kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili ya kuwasaidia vijana suala la ajira.Risala iliyosomwa kwa mgeni rasmi imeeleza Halmashauri ya Ubungo imeidhinisha kutoa fedha kwa vikundi 364 ambapo vikundi 119 ni vya vijana na vikundi 245 ni vya wanawake.Jumla watakaonufaika na mikopo hiyo ni wananchi 11,312.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Joseph Kakinda akiwa ameambatana na viongozi wa Ubungo wakitembelea mabanda ya wajasiria mali mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya wakina Mama na Vijana,walemavu leo jijini Dar as Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Joseph Kakinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ubungo wakitembelea katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya wakina Mama na Vijana,walemavu leo jijini Dar as Salaam.

Hivyo makala UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA
yaani makala yote UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/ubungo-yapongezwa-kwa-utoaji-mikopo-kwa.html
0 Response to "UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA"
Post a Comment