Loading...
title : WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO
link : WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO
WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFC) Profesa Dos Santos Silayo amesema ipo haja kwa Watanzania kuhakikisha wanatunza mikoko na kufafanua kuwa mikoko imekuwa ikichukua hewa ukaa mara 10 zaidi ya mimea mingine.
Ametoa kauli hiyo leo wakati wa upandaji miti ya mikoko katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam na kufafanua Wakala wa Misitu Tanzania wataangalia namna ya kufanya kwa kushirikiana na wadau wengine ili kwenye maeneo ya mikoko wananchi ambao wamekuwa wakiipanda na kuitunza mikoko kujipatia kipato kwa kufuga nyuki.
Pia Prof.Silayo amesema katika Taifa la Tanzania wanatoa msukumo wa kuifanya nchi kuwa kijani kwa kuendelea kuhifadhi maeneo ambayo yamehifadhiwa yaendelee kutunzwa, kupanda miti maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na miti na maeneo ambayo yalikuwa na miti na ikaharibiwa basi ni kupanda miti mingine huku akielezea pia kuitunza miti iliyopo.
"Kwa kufanya hivyo nchi itaendelea kuwa ya kijani kama ambavyo ilivyo kauli mbiu ya kuifanya dunia kuwa ya kijani ambapo kwa Tanzania kupitia Wakala wa Misitu Tanzania tumekuwa tukichukua hatua mbalimbali ikiwamo ya kuhifadhi misitu iliyopo,"amesema.
Akizungumzia mikoko Prof.Silayo amefafanua ni furaha yake kwamba misitu ya mikoko ndio ya kwanza kuhifadhiwa ambapo ametoa historia kuwa ilianza kuhifadhiwa mwaka 1920 na kwa Tanzania ikaanza kuhifadhi miaka nane baadae.
Amesema nchi 121 duniani ndizo zenye mikoko na Tanzania ni ya tisa kwa kuwa na mikoko mingi ikitanguliwa na nchi ya Nigeria.
"Miti ya mikoko ina faida nyingi ikiwamo ya kusaidia kuzuia mmomonyoko kati ya bahari na nchi kavu. Robo ya watu duniani wanaishi karibu na bahari na hivyo mikoko husaidia kuepusha jamii hiyo kutoathirika na mawimbi ya mvua,"amesema Profesa Silayo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos Silayo akizungumza leo wakati wa upandaji miti uliofanyika katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka , Globu ya jamii)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu, Profesa Dos Santos Silayo (wakwanza kulia alievaa kofia) pamoja na wadau mbalimbali wa Mazingira wakipanda miti katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu, Profesa Dos Santosa Silayo akimsikiliza Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Mazingira Mbweni, Husna Hussein wakati akielezea upandaji wa miti ya mikoko ambayo wamekuwa wakipanda tangu mwaka 1998.
Upandaji wa miti ya mikoko ukiendelea katika eneo la Mbweni Jijini Dar Es Salaam
Hivyo makala WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO
yaani makala yote WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/wakala-wa-misitu-tanzania-wazungumzia.html
0 Response to "WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO"
Post a Comment