Loading...

WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA

Loading...
WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA
link : WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA

soma pia


WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA

Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

WANAFUNZI zaidi ya 600 wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumkambati Kata ya Nyamidaho wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wanalazimika kusoma katika chumba kimoja kutokana na uhaba wa madarasa na wingi wa wanafunzi.

Hali hiyo imewalazimu wazazi kuanzisha ujenzi wa shule nyingine Katika vijiji jirani vya Kumtundu na Mkuyuni.Hayo yalibainika jana wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akitembelea miradi ya Wilaya hiyo ilioanzishwa na wananchi na inayofadhiliwa na Serikali.
Ambapo alifika katika Shule ya Msingi Kumtundu iliyoanza kujengwa kwa juhudi za wananchi wa kijiji hicho ili kupunguza wingi wa wanafunzi katika shule iliyopo katika Kijiji jirani cha Mvungwe.

Akitoa taarifa ya shule hiyo Mkuu wa Shule ya Msingi Kumkumbati Falesi Lugati amesema hhule hiyo inajumla ya wanafunzi 2024 na jumla ya walimu 14 na darasa la tatu ndilo lina wanafunzi 600, ambapo wanalazimika kuwagawa awamu mbili ya asubuhi na mchana kwa lengo a kuwaweze kuwafundisha na kumpunguzia mzigo mwalimu anaefundisha darasa hilo .

Amesema shule hiyo inahudumia wanafunzi wa vijiji viwili na wameanza kutatua tatizo la mrundikano wa wanafunzi kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa, na wananchi wa Kijiji cha Mkumtundu wameanza ujenzi wa shule mpya itakayo saidia kupunguza wanafunzi waliopo katika shule hiyo kuhamia katika shule jirani inayojengwa.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule hiyo Katibu wa kamati ya ujenzi wa Shule ya Msingi Kumtundu Raphael Zacharia amesema wameanza ujenzi wa madarasa manne na ofisi moja na ujenzi wa msingi na ukuta pamoja na upauaji umekalika na jumla ya ghalama ni Sh. milioni 14 na Sh.milioni 11 zimechangwa na wananchi na Waziri wa Elimu alichangia Sh. milioni tatu. 

Amesema changamoto ni upungufu wa vifaa vya ujenzi uhaba wa kifungu cha fedha kuwalipa mafundi na kuomba Serikali kuunga mkono kuchangia vifaa vya ujenzi ili kukamilisha ujenzi pamoja na upatikanaji huduma za maji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti aliwapongeza wananchi kwa hatua hiyo waliyoichukua ya kuona upungufu wa vyumba vya madarasa na kuona wanafunzi wanavyoteseka na kuamua kutafuta shule nyingine ili kutatua tatizo la wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya shule.

Amesema ataendelea kuhimiza fedha inayotakiwa kutolewa kwa ajili ya kumalizia shule hiyo ianze, na kuahidi kuchangia Sh.milioni mbili kutoka katika Mfuko wa Mkuu wa Wilaya ili kuiongezea kwenye vifaa ambavyo bado havija nunuluwa.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Godfrey Kasekenya amesema wamejipanga shule hiyo inakamilika Januari mwaka 2019 wanafunzi wanaanza kusoma na wao kama halmashauri wamejiandaa kukamilisha matundu 10 ya vyoo kupitia mfuko wa EPFORR kiasi cha Sh. milioni nane zimetengwa kwaajili ya shughuli hiyo.

Brigedia Jenerali Gaguti alitembelea vituo viwili vya Afya vya Nyamidaho na Nyakitonto Vituo vya Afya vinavyo jengwa kwa fedha za Serikali Kuu kwa kutuma uraratibu wa Force Account ambapo aliwapongeza viongozi wa vijiji na wananchi kwa kujitolea kukamilisha ujenzi huo kwa gharama nafuu na kazi inaendelea vizuri na kuwataka Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za maendeleo.



Hivyo makala WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA

yaani makala yote WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/wanafunzi-zaidi-ya-600-wa-darasa-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA"

Post a Comment

Loading...