Loading...
title : WATAALAMU WA MASULA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI
link : WATAALAMU WA MASULA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI
WATAALAMU WA MASULA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI
Mkufunzi wa Masula ya Uongozi na Menejimenti katika Maabara, Mayala Lushina akitoa mafunzo kwa wataalamu wa Maabara za afya juu ya utaratibu na mikakati ya Urasimishwaji katika Chuo cha Maabara Muhimbili.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Serikali imewaagiza wamiliki wa maabara binafsi kote nchini kuzingatia na kufuata taratibu zilizowekwa katika kutoa huduma ili kufikia viwango vinavyohitajika katika sera ya utoaji huduma za afya.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa Mahabara binafsi za Afya, Dikson Majige alipokuwa akifungua mafunzo ya kuelimisha wataalamu wa maabara kuhusu taratibu na mikakati ya urasimishwaji.
Majige amesema kuwa mafunzo hayo yatumike katika kutekeleza mikakati mipya ya kudumu ya huduma za maabara za afya katika kazi zao.
“mafunzo haya yatumike kutekeleza kazi kwa juhudi ,maharifa na uaminifu mkubwa kufanikisha usimamiaji mzuri wa maabara za afya nchini na kutoa huduma zenye ubora na viwango vya kimataifa” amesema Majige.
Amewataka kila mmoja kufanya tathmini ya huduma anayotoa hili kujijua kuwa kama anawajibika ipasavyo katika utendaji wake wa kazi.
Amesema kuwa wamiliki na wasimamizi wa huduma za maabara wajiweke tayari kutoa huduma bora Zaidi ambazo zitakuwa mfano kwa wengine.
Mwenyekiti wa Institute of Laboratory (EA) Limited , Sabas Mrina akizungumza na Wataalamu wa Maabara za afya umuhimu wa wao kurasimishwa na mamlaka za serikali.
Mkufunzi wa utambuzi wa bidhaa na vifaa bora vya Maabara Colman Msuya, akiwaeleza wataalamu hao wa Maabara za Afya umuhimu wa kukagua vifaa vyao kabala yakuanza kutumi ahili kuepuka kupata majibu yasiyo sahii kwa kutumia vifaa visivyo na ubora.
Wataalamu wa Maabara wakifatilia somo Kuhusu utaratibu na mikakati ya urasimishwaji wa maabara za afya katika Shule ya Maabara Muhimbili
Hivyo makala WATAALAMU WA MASULA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI
yaani makala yote WATAALAMU WA MASULA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAALAMU WA MASULA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/wataalamu-wa-masula-ya-maabara-waagizwa.html
0 Response to "WATAALAMU WA MASULA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI"
Post a Comment