Loading...

WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO

Loading...
WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO
link : WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO

soma pia


WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani.

ASILIMIA 48 ya wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) hawajapima kujua afya zao ambapo asilimia 52 pekee walio na virusi hivyo ndio wanaodaiwa kupima kubaini hali zao.

Aidha imeelezwa watu 81,000 Tanzania wanaambukizwa maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa mwaka, watu 200 wanaambukizwa maambukizi hayo kwa siku,ambapo kati yake 50 ni vijana.

Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) ,Leonard Maboko aliyasema hayo,wakati akifungua mkutano wa mpango mkakati wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwa kushirikiana na waandishi wa habari,Mjini Kibaha,Pwani.

Alisema ukimwi bado ni tishio na ni ajali kama zilivyo ajali nyingine ambayo haionekani lakini ni ajali mbaya kutokana na kusababisha maambukizi mapya kila siku kwa watu 200 idadi ambayo sio ndogo.“Kutokana na hali hii kuna malengo ya kitaifa mawili iikiwemo kuwa na 90 tatu, ambapo asimilia 90 ya kwanza ni ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ambao bado hawajajitambua afya zao kuhakikisha wawe wamepima ifikapo mwaka 2020”alisema Maboko.

Pia ,wanaoishi na virusi vya ukimwi ifikapo 2020 wawe wameingia katika kutumia dawa za kufubaza VVU na ifikapo mwaka huo asilimia 90 ya ambao wanatumia dawa hizo wawe na virusi vilivyokuwa tayari vimefubaa.Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,lengo jingine ni kutimiza 000 na ifikapo 2030 kuondoa maambukizi mapya ya UKIMWI,Unyanyapaa na Vifo.“Malengo ya 90 tatu ,kwa Tanzania 90 ya kwanza ina shida , tunafanya vizuri katika 90 ya pili na ya tatu ambapo 90 ya pili tuna asilimia 91 tunafanya vizuri, kuwa watanzania waliopima wamehakikisha wanatumia dawa,na 90 ya tatu ni asilimia 88 ambayo walianza dawa na kufubaza virusi .

Maboko ,alisema 90 ya kwanza ya kuhakikisha walio na virusi wanapima hali zao hatufanyi vizuri kwani wanaojitokeza kujua hali zao hawajitokezi.Alielezea asilimia 52 ya walio na virusi waliopima hali zao waliweza kujibaini wakati asilimia 48 hawajui afya zao.“Kwa kutumia kalamu zenu tusaidieni hili,mtusaidie kutoa elimu,kuhamasisha watu wakapime ,na tunatarajia kuanza kampeni za uhamasishaji ,tukumbushane kwani ugonjwa huu una dawa za kufubaza virusi hivyo endapo utagundulika kuambukizwa”alisisitiza Maboko.

Pamoja na hayo,alisema Tume hiyo, inatarajia kuanza kampeni za kitaifa kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya kujitokeza kupima kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo walioaminika kuwa na VVU ndio waliopima kujua hali zao.Alisema ,kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na itakuwa endelevu hadi hapo watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza gonjwa hilo .

Maboko alisema ,wale watakaobainika kuwa na maambukizi mapya watatakiwa kuanza tiba ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) mapema ili kuondoa vifo vinavyotokana na virusi hivyo .“Asilimia 45 ya wanaume ndio wanaoaminika kuwa wamepima na kujua hali zao ,hali ambayo inaonyesha ni kiwango cha chini “.Hata hivyo Maboko alisema ,maambukizi mapya ya ukimwi yanaongezeka zaidi kwa kundi la vijana hususan wa kike .“Hii inaonyesha huko kipindi cha nyuma hakukuwa na hali hiyo hivyo haina budi kundi hilo likatiliwa mkazo ,ili kupunguza ongezeko hilo “

Maboko alisema katika kundi la vijana, kati ya watu kumi wenye maambukizi mapya kwa mwaka ,vijana wanne sawa na asilimia 40 ugundulika kupata maambukizi hayo.Alielezea, kati ya vijana kumi waliopata maambukizi mapya kila mwaka nane huwa vijana wa kike na wawili ni vijana wa kiume.Alisema, mwaka 2016/2017 walifanya utafiti ambako walitembelea kaya 15,505,ambapo walihoji na kupima wanawake 19,852 , wanaume 16,235 na watoto wenye umri wa miaka 0-14 waliopo 10,452 .

Maboko alisema kwamba, wanawake asilimia 95 walikubali kuhojiwa na kupimwa ,wanaume asilimia 85 walikubali na watoto asilimia 92 waliohojiwa na kupimwa.“Miaka yote tulikuwa tukifanya utafiti na kupima miaka 15 hadi 49, hii ni mara ya kwanza kuanzia miaka 0-64”alisema Maboko.Hali ya maambukizi ya ukimwi Tanzania kwasasa ni asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.1 ,hali inapungua lakini inatakiwa kuendelea kupambana na maambukizi mapya ,na Tanzania bila ukimwi inawezekana”.
Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Leonard Maboko ,akionekana akizungumza jambo.(picha na Mwamvua Mwinyi)


Hivyo makala WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO

yaani makala yote WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/watu-200-wanaambukizwa-vvu-kwa-siku50.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO"

Post a Comment

Loading...