Loading...
title : Balozi Dkt. Asha Rose Migiro azindua Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza
link : Balozi Dkt. Asha Rose Migiro azindua Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza
Balozi Dkt. Asha Rose Migiro azindua Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza
Jumamosi tarehe 23 Juni, 2018 Mhe. Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association of Tanzanians in the UK.Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za Diaspora kutoka mikoa mbalimbali ya Uingereza na wanachama wa kujitegemea.
Wajumbe wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa “UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.
Akihutubia hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia kwa ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
Mhe Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini Dr Asha Rose Migiro akikata cake katika uzinduzi wa Jumuiya Kuu ya Watanzania Uingereza sherehe hizo zilizofanyika mjini Reading na kuhudhuriwa na mamia ya Watanzania pamoja na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza Tanzania nchi iliojaliwa amani na utulivu katika Africa. Kutoka kushoto ni Joe Warioba Kamati Maalum, katikkati Mhe Balozi Asha Rose Migiro, Dr Donald Mlewa, na Bi Neema Kitilya Kamati Maalum. Lengo la Jumuiya na Kauli mbiu ya Watanzania wa Uingereza ni "Umoja ni Nguvu na Tanzania ya Viwanda inawezekana 'Watoto wakitumbuiza kwa wimbo maalumu
Sehemu ya waliohudhuria sherehe hizo
Wanajumuiya wakiwa kwenye sherehe hizo
Ukumbi ulijaa
Hivyo makala Balozi Dkt. Asha Rose Migiro azindua Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza
yaani makala yote Balozi Dkt. Asha Rose Migiro azindua Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Dkt. Asha Rose Migiro azindua Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/balozi-dkt-asha-rose-migiro-azindua.html
0 Response to "Balozi Dkt. Asha Rose Migiro azindua Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza"
Post a Comment