Loading...
title : BARAZA LA MADIWANI URAMBO LATOA MWEZI MMOJA KWA WATENDAJI KUJIBU HOJA ZILIZOBAKI ZA CAG
link : BARAZA LA MADIWANI URAMBO LATOA MWEZI MMOJA KWA WATENDAJI KUJIBU HOJA ZILIZOBAKI ZA CAG
BARAZA LA MADIWANI URAMBO LATOA MWEZI MMOJA KWA WATENDAJI KUJIBU HOJA ZILIZOBAKI ZA CAG
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Robert Makungu akitoa ufafanuzi wa baadhi wa maeneo wakati kikao maalumu cha kuwalisha taarifa ya ukaguzi wa Hesabu na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hasabu za Serikali kwa mwaka ulioshia Juni 30, 2017 kilifanyika leo mjini Urambo.
Na TIGANYA VINCENT , RS TABORA . Mwamba wahabari
WATENDAJI mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wamepewa Mwezi mmoja kuhakikisha wanajibu hoja 86 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hasabu za Serikali ambazo hazijapata majibu hadi hivi sasa ili ziweze kufungwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi kwa niaba ya Baraza hilo wakati akifunga kikao maalumu cha kuwalisha taarifa ya ukaguzi wa Hesabu na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hasabu za Serikali kwa mwaka ulioshia Juni 30, 2017.
Alisema ndani ya muda huo kila Mkuu wa Idara ambayo hoja imeelekezwa kwake ni lazima ajikite katika kutafuta majibu ikiwa ni pamoja na kutafuta vielelezo ambavyo vinatakiwa na CAG ili hoja ziweze kufungwa na kumalizika.
Malunkwi alisema ucheleweshaji majibu ya hoja zilizotolewa utapelekea kuongezeka na hoja nyingine na kuna uwezekano wa kuzalisha hati chafu , jambo ambalo sio zuri.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maoni yake katika Baraza hilo , alisema ni vema Watendaji wakahkikisha wajitahidi kufanyakazi kwa umakini ili kuzuia uzalishaji wa hoja mpya na sio kujiandaa zaidi kujibu hoja.
Alisema kila Mkuu wa Idara akisimama katika nafasi yake na kutumia utaalamu wake na kulishauri vizuri Baraza hakutakuwepo na hoja tena, kasoro zile ambazo zitakuwa nje ya uwezo wao kama vile uhaba wa watumishi.
Aidha Mkuu wa Mkoa aliwataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia vizuri watendaji na kwa kuzingatia ushauri watakaopewa ili Halmashauri hiyo iendelee kuwa na Hati safi.
Kwa upande wa Mkaguzi Mkuu wa Nje kutoka Ofisi ya CAG Mkoani Tabora Mohamed Msangi alisema utekelezaji wa maoni ya CAG sio wa kuridhisha kwani Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ilikuwa na hoja 116 na ilijibu 30 ambazo zifungwa na kubaki 86 ambazo hazina majibu.
Alisema kati ya hoja hizo zilijumuisha hoja za miaka ya nyuma.
Hivyo makala BARAZA LA MADIWANI URAMBO LATOA MWEZI MMOJA KWA WATENDAJI KUJIBU HOJA ZILIZOBAKI ZA CAG
yaani makala yote BARAZA LA MADIWANI URAMBO LATOA MWEZI MMOJA KWA WATENDAJI KUJIBU HOJA ZILIZOBAKI ZA CAG Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA MADIWANI URAMBO LATOA MWEZI MMOJA KWA WATENDAJI KUJIBU HOJA ZILIZOBAKI ZA CAG mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/baraza-la-madiwani-urambo-latoa-mwezi.html
0 Response to "BARAZA LA MADIWANI URAMBO LATOA MWEZI MMOJA KWA WATENDAJI KUJIBU HOJA ZILIZOBAKI ZA CAG"
Post a Comment