Loading...
title : KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA
link : KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA
KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeipiga kalenda kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Msanii na mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu na wafanyakazi wake hadi Juni 19 mwaka 2018.
Kesi hiyo ilikuja leo kwa ajili ya Wema na wenzake kuanza kujitetea Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba huku upande wa Wakili wa Serikali Costantine Kakula na Wakili wa utetezi Albert Msendo wakiwa wapo tayari kuendelea na kesi.
Hata hivyo, Hakimu Simba anayesikiliza kesi hiyo amepata udhuru kikazi na kulazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 19 mwaka 2018 ambapo washtakiwa wataanza kujitetea.Kesi hiyo imefikia hatua hiyo baada ya Hakimu Simba kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.
Na kutoa uamuzi ambapo aliwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu na hivyo wanapaswa kujitetea.Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.Inadaiwa kuwa Februari 4 mwaka 2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.
Hivyo makala KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA
yaani makala yote KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/kesi-inayomkabili-wema-sepetu-yapigwa.html
0 Response to "KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA"
Post a Comment