Loading...

MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU

Loading...
MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU
link : MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU

soma pia


MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU

Na Stella Kalinga, Simiyu
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma amewaongoza wananchi na viongozi wa CCM na Serikali wa mkoa wa Simiyu katika mazishi ya aliyewahi kuwa mbunge wa Bariadi, Mkuu wa Wilaya katika maeneo mbalimbali hapa nchini,ambaye pia alikuwa Katibu wa Itikadi  na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw. Danni Makanga, ambayo yamefanyika katika Mtaa wa  Kidulya Mjini Bariadi .

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Gachuma ametoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huo, huku akiwaasa ndugu na familia kuendelea kuishi maisha ya umoja na kushirikiana.

Aidha, Gachuma amepongeza mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano uliopo kati ya Viongozi wa Chama na Serikali katika masuala yote ikiwa ni pamoja na misiba na akikiri kuwa yeye pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wake(Mara) walioongozana naye wamejifunza jambo hilo kutoka Simiyu.

"Napenda niupongeze uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa namna  mnavyoshirikiana, msiba wa ndugu yetu Makanga mmeubeba wote kwa pamoja  tumeona kuna umoja na ushirikiano kati ya viongozi wa Chama na Serikali hili ni jambo jema sana ,  bahati nzuri nimefuatana na Katibu Mwenezi wangu wa Mkoa utaratibu huu na sisi tunaubeba kama somo" alisema Gachuma.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa salamu za rambirambi ametoa pole kwa familia na kuwaomba ndugu na familia waendelee kuwa wamoja na wasikubali kugawanywa kwa namna yoyote, huku akielezea kuwa CCM imempoteza mtu muhimu makini sana ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika Chama, Serikali na Taifa kwa ujumla.
 Vijana wa Green Guard wa CCM akiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga kuelekea eneo la mazishi ambayo yamefanyika katika Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi Mkoani humo.
 Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga likiteremshwa kaburini kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika katika Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi Mkoani humo
 Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, . Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga Mjini Bariadi.
 Kutoka kulia  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma wakiweka udongo katika kaburi alizikwa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga amabye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi.
 Kutoka kulia  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kupitia Mkoa wa Simiyu, Gungu Silanga na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Busega, mhe. Tano Mwera na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga Mjini Bariadi.
 Padri wa Kigango cha Mtakatifu Michael Kidulya, Parokia ya Mtakatifu Luka Bariadi, James. Kitasanja akitoa mahubiri katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa la aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU

yaani makala yote MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mjumbe-wa-nec-gachuma-awaongoza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU"

Post a Comment

Loading...